Mada: vifo vya gafla kwa kuku
Mada: vifo vya gafla kwa kuku Nimatumaini yangu ndugu msomaji, u mzima wa afya njema kwa kadri Mungu alivyokujalia kuamka salama. Ni muhimu kwangu kuhakikisha unapata taaeifa sahihi kuhusiana na ufugaji wa kuku aina zote. Leo nimependa kukuletea somo muhimu sana kwako kama linavyojieleza hapo juu. Niingie moja kwa moja kwenye somo la leo, kuku ni ndege mchangamfu sana katika ubora wa afya yake. Mara nyingi kuku akiwa anaumwa kuna dalili mbalimbali atazionyesha ili kama mfugaji ukiwa makini ni rahisi kutambua na kumsaidia au kumtibu. Zifuatazo ni dalili mbalimbali ambazo utaziona kwa kuku wako ili ujue ni ugonjwa gani . 1.Kuku kuzubaa ni moja ya dalili isiyo ya kawaida kwa kuku. Mara zote kuku ni mchangamfu sana kufikia kwamba hawezi tulia sehemu moja. Kwa hiyo ukiona kuku wako amezubaa kwa muda mrefu ujue kuna tatizo, hivyo ni muhimu kuchunguza tatizo ni nini ili uweze kumtibu kwa wakati kabla madhara makubwa kutokea. Mfano, siku moja nilikuta kuku wangu kazubaa. Ikabidi n...