Je unajua ni vitu gani muhimu katika ujenzi wa banda bora tupe maoni yako nasi tukufungue sasa

UJENZI WA MABANDA BORA YA KUKU : Banda lifaalo lazima liwape kuku mazingira mazuri na kuwalinda dhidi ya hali mbaya ya hewa (mvua, upepo na jua). Hakikisha banda lina nafasi ya kutosha kwa kuku wanaofugiwa humo.
– Uwiano mzuri wa kuku kwa eneo ni futi mraba moja kwa kuku wa mayai, na futi moja ya mraba kwa kuku wa nyama. Kwa sehemu za tropiki mabanda yawe wazi sehemu za juu ili kuruhusu mzunguko wa hewa, Pia liwe na mwelekeo wa mashariki-magharibi ili kupunguza kiasi cha mwanga wa jua kuingia moja kwa moja katika banda.
– Ni muhimu banda iwe muonekano wa mstatiri na ukuta wenye kimo kisichozidi futi tatu kwa upande mrefu. Ukuta huu unaweza kutengenezwa kwa mabati yaliyokatwa au mbao za rangi ya fedha au matofali. Pande zilizobaki za kuta ziwekwe wavu wa waya. Paa la banda lazima liweze kuakisi mwanga na joto. Haya yote yatasaidia katika kuhakikisha kwamba banda liko katika hali nzuri linastahili kufugia.
– Sakafu imara ya sementi ni bora kwa sababu ni rahisi kusafishwa. Lazima kuwepo bafu lenye kipukusi cha kutakasa miguu katika mlango wa kuingilia ili kuua vijijidudu wakati kuku waingiapo ndani. Ili kupunguza hatari ya panya kuingia katika banda la kuku ni muhimu kusafisha majani yote kuzunguka banda kwa upana wa mita 3 hadi 5.
– Ghala la chakula litengwe mbali na banda. Banda la kuku lijengwe katika sehemu iliyojitenga ili kupunguza uwezekano wa maambukizo. Milango ifungwe wakati wote kuzuia watu kuingia ovyo. Tundu za wavu wa kuzungushia banda la kuku ziwe ndogo kuzuia uharibifu wa wanyama na ndege mfano, ndege wa porini, paka, mbwa na panya. Ni muhimu kuwatenganisha kuku kulingana na umri, hii husaidia kupunguza uwezekano wa kuenea kwa magonjwa.
– Katika ufugaji kuku utaratibu “ndani wote -nje wote “ ni mzuri kwa sababu unapunguza uwezekano wa kuzaliana kwa vijidudu visababishavyo magonjwa. Pale ambapo mkulima anataka kufuga kuku wa umri tofauti, vema kila kundi la rika moja liwekwe katika nyumba ya peke yake.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa