JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

Hizi ni baadhi ya njia ya kuikinga na Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles.
Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki 4 hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani.
Bawasiri husababishwa na nini

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu:
  1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
  2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
  3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
  4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
  5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
  6. Kuharisha sana kwa muda mrefu
  7. Kutumia vyoo vya kukaa
  8. Kunyanyua vyuma vizito
  9. Mfadhaiko/stress
  10. Uzito na unene kupita kiasi nk
Dalili za bawasiri
  1. Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
  2. Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
  3. Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
  4. Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
  5. Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote
Matibabu ya bawasiri:
Kutegemea na umri wako na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja kati ya hizi zifuatazo. Kumbuka kumshirikisha daktari wako kabla ya kuamua kuzitumia hizi dawa.

Bawasiri na tiba zake
1. Habbat-Sawdaa

Dawa nyingi zinazotumika kutibu bawasiri zina madhara mengine mabaya na nyingi ya hizo hazitibu kabisa bawasiri na kulazimisha wengine kufanya upasuaji.
Mafuta ya habbat soda kwa upande wake yanatoa suluhu ya haraka katika kutibu bawasiri zote ya nje nay a ndani na tafiti zinaonyesha yanao uwezo wa kuzuia kusambaa au kuongezeka kwa ugonjwa huu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa sehemu yenye tatizo nje na ndani kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa





2. Habbat-Sawdaa na Asali

Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya masaa manne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida.
3. Aloe Vera Fresh

Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu.
Jipake nyingi tu na uiache hivyo masaa kadhaa au mpaka utakpaoenda kuoga tena.
Tengeneza pia juisi freshi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi 1 kutwa mara mbili kwa wiki 3 hadi 4.

.
4. Unga wa Majani ya Mlonge

Bawasiri ni ugonjwa unaoanzia ndani ya tumbo kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula. Ukiugua bawasiri ujuwe kuna kitu si sawa ndani ya tumbo lako. Bawasiri ni ishara ya moja kwa moja kwamba kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kuna tatizo.
Mara nyingi bawasiri inaanza kwa mtu kupata choo kigumu au kufunga choo kabisa kwa siku kadhaa. Ukitumia mlonge utapata choo kizuri na kilaini na siyo rahisi upate tatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kama unatumia mlonge.
Mlonge unaboresha afya yote ya mwili kwa ujumla, unaondoa msongo wa mawazo na kukufanya ujisikie vizuri tena. Mtu yeyote anayesumbuliwa na bawasiri pamoja na dawa zingine mlonge lazima atumie ili kupata uponyaji wa hakika na wa kudumu.
Vitamini B1 (Thiamine) na vitamini B2 zipatikanazo kwenye mlonge husaidia mwili wako kubadili wanga kuwa nguvu ndani ya mwili wako.
Kazi hii ni mhimu katika uundwaji na utengenezaji upya wa seli ndani ya mwili. Vitamini hizi mbili pia zina umhimu mkubwa katika kuweka sawa hisia za njaa. Vitamini B3 na folic asidi (niacin) ni moja ya vitu mhimu kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Vitamini hizi zinasaidia katika kuvunjavunja chakula hasa vyakula vya wanga na mafuta kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. This vitamin will aid in efficient breakdown of carbohydrates and fats. Vitamini B6 (Pyridoxine) husaidia kushughurikiwa (kumeng’enywa) kwa protini yote iliyomo kwenye chakula.
Vitamini H (Biotin) husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuzalisha kolesto, kuishughurikia protini, mafuta na wanga. Baada ya protini kuwa imemeng’enywa, vitamini H husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuuondolea sumu na taka nyingine zisizohitajika.
Vitamini za kundi B nyingi zinaweza kuongezwa mwilini kwa kutumia vyakula ambavyo havijakobolewa, bidhaa za maziwa ya ng’ombe, maharage, maharage ya kijani na samaki wa baharaini. Kwa mjibu wa utafiti, watu wengi hawapati vitamini hizi kiasi cha kutosha kwenye milo yao kila siku.
Vitamini C inajulikana kwa umhimu wake wa kuweka meno na fizi kuwa vyenye afya zaidi ambavyo kama matokeo yake ni afya bora ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vitamini C inasaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kutokana na ukweli kwamba ndiyo vitamini inayohusika na umeng’enywaji wa chuma mwilini.
Ikiwa utajumuisha matunda mengi yenye vitamini C kwenye chakula chako ile nyuzinyuzi (faiba) ndani yake inasaidia kuondoa matatizo mbalimbali kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Nyuzinyuzi zinasaidia kuondoa sumu mbalimbali ndani ya mwili.
Mlonge una vitamini C mara 7 ZAIDI YA ILE INAYOPATIKANA KATIKA MACHUNGWA!
Vitamini D husaidia kujenga meno imara ambayo ni mhimu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini D unaweza kupelekea mtu kupata saratani ya utumbo mpana.
Unaweza kupata vitanini D kwa wingi kwa kutumia zaidi mlonge.
Vitamini na viinilishe vingine unavyopata toka kwenye mlo kamili ni mhimu kwa ajili ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula. Unapokula kiasi kingi cha wanga na mafuta mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unazidiwa kazi na hautaweza kuwa na afya nzuri.
Unahitaji chakula chenye vitamini nyingi za kutosha ambazo ni mhimu kwa afya ya mwili.
Kwa kuongezea mlonge una lundo la vitamini kundi B kuliko mti au mmea mwingine wowote unaoufahamu.
Mlonge una vitamini B, B1, B2, B3, B5, B6, B12, D, E, K, folic acid, Kalsiamu (mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe), madini ya shaba, potasiamu, magnesia, kromiamu na vitamini, na madini madogo madogo mengine mengi mhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.
Mlonge pia una zile amino asidi mhimu 9 za kwenye protini.
Elewa tu kwamba mti huu wa maajabu mti wa mlonge na majani yake mti ambao hujulikana pia kama mti wa uzima una viinilishe bora na mhimu zaidi kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili ambavyo siyo rahisi kuvielezea vyote kimoja baada ya kingine
Kutibu bawasiri tumia unga wa majani ya mlonge kijiko kidogo kimoja cha chai kwa mwezi mmoja mpaka miwili ndani ya juisi ya matunda (hasa juisi ya parachichi) au katika uji au kwenye mtindi kutwa mara moja.
Usisahau pia kunywa maji ya kutosha kila siku, kufanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama (squatting) ili kuwa na kinga imara ya mwili wako.
Unga wangu wa majani ya mlonge ni mzuri na naweza kusema pasipo na hofu kuwa huwezi kupata sehemu nyingine wenye ubora unaokaribia na wangu. Ninauandaa kwa umakini mkubwa ili ubaki na viinilishe vyake na ni wa kijani kweli kweli

5. Juisi ya limau (lemonade)

Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limau sifa yake kuu hapa ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwakuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:
*Chukua asali mbichi nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita.
*Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.
*Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalasini lita 2 na nusu ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5, chuja vizuri. Ihifadhi katika friji isiharibike.
Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 30 hivi kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri.
Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
Unaweza pia kupakaa sehemu yenye bawasiri juisi hii ukitumia pamba kutwa mara 2. Unaweza kusikia maumivu zaidi lakini pole pole yataacha.

6. Siki ya tufaa

Chukua kipande cha pamba na ukichovyo ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na ujipake kidogo kidogo eneo lenye uvimbe taratibu. Unaweza kusikia maumivu zaidi lakini jipe moyo taratibu yatapotea. Hakikisha unapata siki ya tufaa ile ya asili kabisa siyo ile iliyopita viwandani.
Pia kama una bawasiri ya ndani yaani ile isiyojitokeza nje na ukaiona kwa macho moja kwa moja unashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa ndani ya glasi ya maji na unywe yote kutwa mara 2. Hii husaidia pia kupunguza maumivu.
7. Mafuta ya nyonyo

Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne hivi.
8. Mafuta ya lozi (Almond oil)

Yana uwezo wa kunyonya na kulainisha bawasiri hasa ya nje. Hivyo yanalainisha hicho kiuvimbe kinachojitokeza sehemu ya haja kubwa pia kuondoa maumivu kama utakuwa ukiyapaka kila siku.
Tumia pamba ukichovya ndani ya mafuta haya na upake sehemu yenye tatizo mara kadhaa kwa siku kwa wiki 3 hata mwezi mmoja.
9. Mafuta ya zeituni

Mafuta ya zeituni (Olive oil) ni moja ya dawa maarufu katika kutibu bawasiri. Mafuta haya yana viuavijasumu na huondoa pia maambukizi (infections). Yanaweza pia kusaidia kuongeza utanukani wa mishipa ya damu. Yanao uwezo pia wa kukausha kinyama cha bawasiri ya nje yakitumika kwa kupaka kwa kipindi kirefu.
Kunywa kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya zeituni kila siku. Pia tumia pamba pakaa sehemu yenye tatizo nje na ndani kutwa mara 2 kila siku mpaka umepona.
10. Kipande cha barafu

Barafu inasaidia kubana mishipa na hivyo kuzuia uvimbe pia kuondoa maumivu kwa haraka.
Chukua kipande cha barafu na ukifunge ndani ya kitambaa kisafi na uweke moja kwa moja sehemu yenye tatizo kwa dakika 10 hivi. Fanya zoezi hili mara kadhaa katika siku. Zoezi hili linaondoa maumivu ya bawasiri na dalili zake.

Comments