SOKO LA SUNGURA

UKWELI KUHUSU SOKO LA SUNGURA
Habari ya majukumu ndugu wafugaji leo katika ukurasa huu nitazungumzia kuhusu soko la sungura hii ni kutokana na maswali ya watu wemgi wanaoniuliza kuhusu soko hasa mahali lilipo. Pia ni kutokana na utafiti niliofanya na kugundua kuwa wafugaji wengi wa sungura changamoto yao kubwa ni upatikanaji wa soko la uhakika la kuuza sungura wao
Kwanza kabisa kabla ya yote napenda mfahamu kuwa soko la sungura ni kubwa kuliko hata idadi ya sungura iliyopo mtaani tatizo kubwa ni jinsi ya kulifikia soko hilo
Katika ufugaji wa sungura soko limegawanyika katika aina tatu tofauti
1.soko la sungura wa mbegu
2.Soko la mkojo na kinyesi cha sungura
3.Soko la nyama ya sungura
1 SOKO LA SUNGURA WA MBEGU\
Hii ni aina mojawapo ya soko la sungura kwa sasa. Mfugaji wa sungura anaweza kuanzisha ufugaji wa wanyama hawa kwa minajiri ya kuzalisha mbegu bora ya sungura na kuuza kwa wafugaji wapya wanaoanza. Hii ni biashara inayolipa sana kwani mara nyingi sungura wa mbegu huuzwa wakiwa bado wadogo wastani wa siku 30 hadi 60 toka kuzaliwa na kwa wastani bei ya sungura mmoja ni kuanzia sh 15000 had 25000 kwa sungura wa kisasa ( umbo kubwa ) kutegemea na sehemu au mfugaji husika
Mfugaji wa sungura anaweza kunufaika na kuongeza kipato kutokana na uzalishaji huu wa sungura wa mbegu
Nb
Uzalishaji wa sungura wa mbegu unaihitaji usimamizi na uangalizi wa hali ya juu hii ni kutokana na kuzuia muingiliano wa vizazi yaani inbreeding ( kuzaliana ndugu)
2 SOKO LA MKOJO WA SUNGURA
Mkojo wa sungura ni bidhaa muhimu sana kwa wakulima kwani inauwezo wa kurutubisha mimea na kufufua ardhi iliyokufa yaani isiyofaa kwa kilimo pia mkojo wa sungura ni dawa nzuri ya kuuwa wadudu waharibifu na wasumbufu wa mazao shambani. Mfugaji wa sungura anaweza kutumia mkojo wa sungura kama kitega uchumi ambapo sungura watamzalishia mkojo kila siku ambao atawauzia wakulima kwa ajili ya matumizi ya shambani.
Wastani bei ya mkojo wa sungura kwa sasa ni kuanzia sh 2000 hadii sh 5000 kwa lita moja ya mkojo kutegemea na muuzaji
Na wastani wa sungura 6 wanaolishwa vizuri kwa siku huweza zalisha lita moja ya mkojo. Mradi wa sungura huweza kujiendesha kwa kutumia mkojo tu iwapo mfugaji atapata soko la uhakika
NINI KIFANYIKE KUPATA SOKO LA MKOJO
MFUGAJI usikae tu nyumbani kusubili soko likufuate unapaswa kulifuata nitakupa mbinu moja ambao nilishawai kuitumia katika kusaka soko la mkojo ni ikafanikiwa
Soko la mkojo wa sungura ni kwa wakulima wa mazao mbalimbali hasa wakulima wa mazao ya bustani kwani ni watumiaji wa mara kwa mara wa madawa ya kuulia wadudu shambani mwao na kwa asilimia kubwa sana wakulima wengi hawajui manufaaa na faida za kutumia mkojo wa sungura shambani mwao hivyo unachotakiwa kufanya ni kuwapa elimu hio bure ya faida za mkojo wa sungura na jinsi ya kuutumia shambani mwake kisha unawapatia mkojo waa bure wa majaribio ili waone matokea yake kila mmoja waweza wapa lita 5 bure nakuhakikishia katika wakulima watano utakaowafanyia hivyo watatu watakutafuta mara ya pili wakiitaji mkojo mwingine hapo ndipo unaanza kufanya biashara
3.SOKO LA NYAMA YA SUNGURA
Lengo hasa kubwa la ufugaji wa sungura ni kwa ajili ya nyama yake na nyama ya sungura ni nyama bora isiyo na rehemu na ni jamii ya nyama nyeupe. Ufugaji wa sungura kwa ajili ya nyama unaweza kumuondoa mfugaji kwenye janga la umasikini kwa muda mfupi sana
Lengo kuu ni sungura kwa ajili ya nyama lakini ni wafugaji wachache sana ambao wamefikia hatua hiii ya kuuza sungura wa nyama bila matatizo wala vikwazo vyovyote. Wafugaji wengi kilio chao kikubwa imekuwa ni upatikanaji wa soko hilo kama nilivyosema awali kuwa soko ni kubwa kuliko idadi ya sungura waliopo mtaaani.
Nyama ya sungura kwa asilimia kubwa inauzwa katika hoteli za kitalii ndani ya Tanzania na hoteli na migahawa ilizopo nje ya nchi hii katika mataifa yaliyoendelea. Katika kufikia soko hili ndipo changamoto kwa wafugaji inapoanzia, kabla sijatoa mbinu unazopaswa kutumia ili kufikia soko hili ieleweke kuwa watu wa mahoteli wanataka uwe na uwezo wa kusambaza muda wote siku zote kwa muda wa mwaka mzima kiwango cha kilo za nyama utazosambaza inategemea na mahitaji ya hotel husika mfano kuna hoteli zinazotaka kilo 20 kwa wiki zipo zinazoitaji kilo 50 kwa wiki na mnasaini mkataba wa mwaka mzimana kwa upande wa oda zinazotoka mfano wapo wanaotaka tani 2 mwa mwezi kwa mwaka mzima yaani oda ni nyingi kuliko sungura wenyewe
Utakuta mfugaji ana sungura wake 200 atalalamika hana soko na anataka umuunganishe na soko lakini kwa oda kama hizo sungura hao hawatoshi hata kusupply kwa muda wa miezi 2 wote wanakwisha na mkataba unavunjika. Pia mtaani kuna sungura wengi ambao sio wazito wenye maumbo madogo kitaalamu sungura hawa tunasem,a uwiano wa nyama na mifupa mifupa ni mingi hivyo hawafai kwa ajili ya masoko kama haya
NINI KIFANYIKE
Ili mfugaji kufikia soko hili kwa urahisi anatakiwa kuwa na uhakika wa uwezo wa kusambaza sungura wake kwa mwaka mzima bila kukosa. Njia rahisi ya kufanikisha hili ni kwa wafugaji wa sungura kuungana na kuwa kitu kimoja wawe na uwezo wa kuzalisha sungura kwa wingi na kwa kiwango sawa (quality and quantity) au mfugaji ajiunge kwenye vikundi vya wafugaji wenzie ambao tayari wameshaanza kufuga na kuuza pia
Pia mfugaji aliyeanza ufugaji wa sungura anaweza kutafuta wafugaji wenzie kadhaa hata kumi kwa kuanzia wanatosha kuanzisha kikundi kitachowasaidia kufikia soko kwa urahisi kwani mnakua na uhakika wa uzalishaji wa sungura wenu kwa kiwango kikubwa na mnapoanza kuuza mnauza kwa mzunguko mkianza na mtu wa kwanza leo mkija kumaliza wa mwisho mnakuta tayari wa kwanza kashazalisha wengine
Ili kuweza kupata hotel ya kuiuzia nyama ya sungura kwa urahisi wafugaji tunapaswa kufanya kitu kinaitwa MARKET TRIAL ( MAJARIBIO YA SOKO ) hii ni mbinu ya urahisi sana ya kupata soko ya bidhaa yoyote ile mbinu hii tumeitumia na imeleta mafanikio makubwa sana
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua hoteli au migahawa  kadhaa iliyokaribu yako kisha unawapelekea nyama ya sungura ya bure hata kwa siku kadhaa ili wafanye majaribio na waangalie quality iliyopo mfano sisi tulichagua hotel 5 tukawapelekea kila hoteli kilo 5 za nyama katika hizo 5 hotel 3 zilitujibu zikiitaji tuanze kuwasambazia nyama kila wiki. Ikumbukwe nia ya kuwa na uhakika wa kuzalisha mwaka mzima ni kwa sababu wamiliki wa mahoteli wakiandia katika menu yao nyama ya sungura basi isiwepo siku Ikakosekana
KWA SASA KILO MOJA YA SUNGURA NI KATIB YA SH 15,000 HADI 20,000
Wafugaji msikate tamaaa sungura wanalipa sana na wanauzika sana kikubwa ni kuongeza uzalishaji na kuacha tabia ya kujitenga . umoja ni nguvu tuungane ili iwe rahisi kwetu kufanikisha mambo
Nb
Ikumbukwe kuwa mradi wa sungura sio mradi wa kichoyo ni mradi unaotakiwa kuhamasishana na kusaidia kwa pamoja ili kufikia masoko makubwa
Asanteni
<a href="http://c.jumia.io/?a=89570&c=329&p=r&E=kkYNyk2M4sk%3d&utm_source=cake&utm_medium=affiliation&utm_campaign=89570&utm_term="><img src="https://jumia.com/affiliate-program/banners/Jumia Kenya/Smart Shopper - Groceries/728X90.jpg"/></a>

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa