MAGONJWA YA KWALE NA JINSI YA KUPAMBANA NAYO

Magonjwa
KWALE ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata KWALE ni typhoid, mafua na kuharisha .
Tiba za asili
Waweza kuwatibu vifaranga au KWALE wako kwa kutumia njia ya asili ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama.
Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa KWALE na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.
Mwarobaini na Aloe Vera:
Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya KWALE. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).
Kitunguu swaumu:
Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya KWALE wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafisha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapo pona.
Maziwa:
Maziwa yanayotokana na ng’ombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu KWALE waliolegea. Mnyweshwe maziwa hayo KWALE anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ng’ombe wanaotibiwa kila mara.
Pia ni muhimu kuzingatia haya👇👇👇
Siyo lazima KWALE waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.
Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu KWALE kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia;
-Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis),
-Fluban,Coridix au Doxyco kutibu mafua (Coryza) na -Esb3,Trisulmycine au Trimazine hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa