UGONJWA WA MINYOO KWA NG'OMBE.
Ugonjwa wa minyoo husababisha hasara kwa mfugaji wa ng'ombe . Utafiti unaonyesha kuwa ng'ombe wengi wanaathirika na minyoo hiyo hupunguza uzalishaji. Aidha utafiti unaonyesha kuwa tatizo la minyoo kwa ng'ombe limeenea hapa nchini kwetu
.
AINA ZA MINYOO.
Minyoo inayoathiri ng'ombe imegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo; Minyoo inayoishia kwenye maini ya ng'ombe (liverflukes).,Minyoo inayoishia kwenye mapafu (lungworms). ,Minyoo mikubwa ya mviringo (large roundworms). , Minyoo midogo ya mviringo (small roundworms).
MZUNGUKO WA MAAMBUKIZI.
Minyoo hupitia njia zifuatazo: ,Mnyama kuambukizwa na mwingine. Kupenya kwenye ngozi ya ng'ombe. ,
Ndama kupata minyoo kupitia kwa mama (ng'ombe) alieathirika kwa minyoo wakati wa kuzaliwa.,
Ng'ombe kula mayai ya minyoo yaliyomo kwenye majani wakati wa malisho. M
Ndama kupata minyoo wakati wa kunyonya maziwa ya ng'ombe aliyeathirika.
DALILI ZA NG'OMBE ALIYEAMBUKIZWA.
- Kupoteza uzito
- Kukosa hamu ya kula
- Kuhara
- Kupungukiwa na damu
- Kuwa na homa
- Afya yake kufifia na hatimaye kufa
- Tumbo kuwa kubwa kupita kiasi (ndama).
TIBA
Wanyama wapewe dawa za kutibu minyoo mara kwa mara. Mfano:
NILZAN ,NILVERM . PIPERAZINE. ANACUR. THIABENDAZOLE. YOMESAN. OXYDOZIDENE
JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI NA KUZUIA MINYOO ISIENEE.
Minyoo hukingwa kwa njia zifuatazo: Kuepuka kulisha ng'ombe
kwenye majani yenye mayai ya minyoo. Ng'ombe wote wagonjwa watibiwe. Epuka kulisha na kunywesha kwenye mabwawa. Usafi wa banda uzingatiwe. Ng'ombe wasiruhusiwe kukanyaga malisho yao hasa kwenye zero grazing.
MADHARA YA MINYOO
. Husababisha upungufu wa damu. Husababisha upungufu wa maziwa. Ng'ombe huweza kufa.
Comments
Post a Comment