UTENGENEZAJI WA WADUDU KWA CHAKULA CHA KUKU

Kijanaendelevu.blogspot.com

NAMNA YAKUTENGENEZA MCHWA KWA AJILI YA KUKU
Mchwa ni chanzo kizuri sana cha protini kwa kuku,mchwa kwa vifaranga wanakua vizuri sana,kwa kuku wanaofugiwa ndani ni vizuri kuwapa mchwa kwa kuwa wanakosa sehemu yakuokota hao wadudu mbalimbali, watu wengi wanaweza kujiuliza ni kwa namna gani watatengeneza mchwa kwa ajili ya kuku wao, 
KANUNI AU HATUA ZAKUFUATA KUTENGENEZA MCHWA
1.andaa mahitaji muhimu yanatakiwa
-kinyesi kikavu cha ngombe au mbuzi
-majani makavu,au mabua ya mahindi,maharage hata maranda unaweza tumia mojawapo au ukachanganya
-chungu,au sufuria au box
2.changanya vitu tajwa hapo juu vyote vizuri 
3.nyunyizia maji kila kilichomo kilowane kiasi

4.weka mchanganyo wako kwenye chombo ulichokiandaa,chungu,sufuria au box
5.chukua chombo hicho kakiweke sehemu ambayo unahisi mchwa wanaweza kupatika mfano,kichuguu,kwenye njia mchwa, sehemu nyingi ya ardhi kavu mchwa wanapatika
6. Acha chombo chako hapa kwa masaa 24, ila chombo umekiweka kwa kukifunika upande mmoja uwe umenyanyuka kidogo kuruhusu hewa kuingia kwenye mchanganyiko
7.baada ya huo muda mchwa wengi watakuwa wamezalishwa ndani ya chombo chako
7. Chukua chombo kwa upesi kwa kukigeuza ili mchwa usirudi aridhini kisha kawape kuku wako,
zoezi hili ni jipesi sana halihitaji wewe kutumia muda mwingi fanya kila siku ili vifaranga na kuku wako wastawi vizuri. Aksante kwa kuwa pamoja nasi tembelea YouTube kijanaendelevu

Comments