HOMA YA NGURUWE

HOMA YA NGURUWE (African Swine Fever)

Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya nguruwe huenea
kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya nguruwe, na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamu na hauambukizwi kwa binadamu. Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa mekundu.

Madhara yake kwa nguruwe yanaweza kuwa makubwa au madogo yasiyoweza kuonekana kwa macho. Homa ya nguruwe haina tiba maalumu wala chanjo inayofaa na hivyo uzuiaji wa ugonjwa huu unategemea sana utambuzi wa
ugonjwa mapema na kisha kuzuia utembeaji wa holela wa nguruwe (karantini).

Maonyo yamekuwa yakitolewa kupitia mikutano ya hadhara na
vyombo vya habari kama magazeti ya kuzuia kutembea kwa mifugo ovyo pamoja na kuzuia kula nyama ya nguruwe kwa kuhofia kusambaa kwa ugonjwa. Ugonjwa huu umekuwa ukitokea mara kwa mara katika nchi yetu na kuathiri mifugo na soko la nguruwe kwa ujumla.

Ugonjwa huu Huenezwa na Virusi na vyanzo vikubwa vya kuenea kwa ugonjwa huu ni pamoja na
 Nguruwe wagonjwa kuchanganyika na wasio wagonjwa
 Kula chakula chenye virusi
 Kupe laini

DALILI
 Homa kali (41°C)
 Kuhema sana
 Kushindwa kula na kutembea
 Rangi ya ngozi hugeuka kuwa bluu au nyekundu
 Kifo baada ya siku 7.
 Kuharisha
 Huenea kwa kasi baada ya kutokea.

TIBA NA KINGA
 Hakuna Tiba wala chanjo
 Nunua nguruwe kwenye mashamba yasiyo na historia ya ugonjwa
 Usafi wa vifaa, banda na mazingira yake
 Nunua vyakula vilivyothibitishwa
 Usitumie masalia toka sehemu zenye ogonjwa
 Tumia dawa za kuua kupe.
 Nguruwe wagonjwa wachinjwe.

MUHIMU:
Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.

Comments