HAYA NDIO MAGONJWA YA SAMAKI

SOMA HAPA MAGONJWA YA SAMAKI

Kuna magonjwa mengi ya samaki yanayosababishwa na fangasi, bacteria, protozoa, parasites, virus na mazingira yenyewe

1. Ichthyosporidium (WHITE SPOTS)

Huu ugonjwa kwa kifupi hujulikana kama ICHI, husababishwa na
fungus ambao huingia kwa kupitia ngozi na kisha kushambulia maini na figo.
Dalili zake ni samaki kuogelea kwa kupindapinda au kivivu, tumbo kuonekana kama halina kitu (hollow) na alama nyeupe nyeupe kwenye mwili wa samaki

Tiba yake ni pottasium per manganate kwenye maji, Phenoxethol 1% kwenye chakula na Chloromycetin kwenye chakula, dawa zote zinapatikana kwenye
maduka (pet shops).
kwa kawaida ICHI wana miznguko miwili ya maisha, akizaliwa
anaogelea na kujishikiza kwenye mwili wa samaki, kisha anashuka chini kwenda kuzaana (replitications)na kurudi kwenye mwili wa samaki tena. Kwenye hatua hii pottasium per manganate ndio inafanya kazi ya kuzuia ICHI kurudi tena kwenye mwili wa samaki

2. KUOZA MKIA NA MAPEZI
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria, dalili zake kubwa ni kuwa na rangi nyekundu au rangi ya udongo (hudhurungi) kama damu imevilia kwenye kona za mapezi na mkia na kisha baadae sehemu hizi hunyofoka na kubakia kibubutu.

Sababu kubwa ni kuumia kunakosababishwa na kujigonga au madume kupigana, 

Tiba yake ni kwa kutumia antibiotics kama tetracycline au
chloramphenicol kiasi cha 20-30mg/l (miligramu 20-30 za dawa kwa lita moja ya maji)au mili gramu 250 (1 capsule) kwa chakula cha gramu 25

3 MINYOOO KWA SAMAKI

Dalili zipo nyingi na zinategemeana na aina ya minyoo aliyonayo samaki Minyoo inayshambulia matamvua na ngozi Tabia ya samaki hubadilika na huonyesha dalili za muwasho kama kujirushrusha na kujikwangua kwenye vitu.

Rangi ya samaki hubadilia kuwa angavu mwenye rangi ya hufifia Hupumua
kwa haraka huku akinyua mifuniko ya matamvua akiweka wazi matamvua
macho pia yanaweza kuathilika na kupoteza uwezo wa kuona Vifo vingi vinaweza kutokea au wakawa na ugonjwa wa muda mrefu bila kufa

Minyoo inayoshambulia ndani (matumbo)
-Uwepo wa majeraha au vidonda kwenye kuta za utumbo
-Minyoo huonekana kwenye tumbo lililovimba
-Minyoo pia yaweza kuonekana ikining’inia sehemu ya kutolea haja kubwa
-Kwa samaki wadogo ukuaji wao huwa hafifu
-Inaweza kusababisha upungufu wa damu

Matibabu ya Minyoo kwa Samaki

Dawa za kutibu minyoo ya samaki kama ilivyo kwa wanyama wengine kama ng’ombe, mbuzi au kondoo inategemea sana aina ya mnyoo alionao samaki. Hivyo ni vizuri kuchukua sampuli ili kujua aina ya minyoo kabla ya kumpa matibabu.

Magonjwa ya ngozi: Praziquantel (2 mg/L, wawekewe dawa kwenye maji na waoge kwa muda mrefu)

Nematodes (Minyoo wa tumbo): Levamisole (10 mg/L)
waoge kwenye maji yenye dawa kwa siku tatu mfululizo

Comments