Posts

Showing posts from April, 2017

JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA WEWE MWENYEWE.

JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA WEWE MWENYEWE. Vyakula vya kuku huweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa Chakula hicho lazima kiwe na chakula hicho lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile wanga, protini, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza wewe kiwe na mchanganyiko wa vyakula ifuatavyo: ▶ Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, pumba, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti. ▶ Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, mchicha majani ya mpapai na nyasi mbichi. ▶ Vyakula vya kujenga mifupa kama vile aina ya madini chokaa mifupa iliyosagwa na chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama kalsiamu na fosforasi husababisha kuku kuwa na matege, vidole kukunjamana. Misuli kufyatuka na kupofuka macho. ▶ Maji ni muhimu ...

usiyoyajua kuhusu incubators

Image
Incubators ni Mashine zinazo tumika kutotoreshea viuombe mbali mabali hasa Ndege, AINA ZA INCUBATORS 1. Forced Air Incubator 2. Still Air Incubators FORCED AIR INCUBATOR - Forced Air Incubators ni mashine yenye Feni kwa ajili ya kutawanya joto ndani ya incubators STILL AIR INCUBATORS - Hii ni mashine siyo kuwa na fane IPI NZURI? - Inashauriwa kutumia/kununua Forced Air Incubators ndo bora kabisa na haiatakusmbua na hatahivyo kwa incubator kubwa karibia zote ni Fored air, na mara nyingi ndogo ndo still air 3. AINZA INCUBATOR KWENYE OPERATION - Manual - Automatic MANUAL INCUBATORS - Hizi hutumia mikono katika kugeuuza mayai na katika maswala mengine kama kucontro joto na kazalika AUTOMATIC INCUBATORS - Hizi hujiendesha kama Computer, kila kitu hufanywa automatically so kazi za manual hupunguza sana - Ukiwa na Incubnator Automatic na ikawa na sehemu ambayo inajiongeza maji automatically basi inaweza hata kata wiki bila kuchungulia mashine yako na ikawa in...

hii ndio maana ya ufugaji huria/free range

UFUGAJI HURIA/FREE RANGE Watu wengi wamekuwa wanauliz kuhusu huu ufugaji wa free range na kutaka kujua ukoje. Huu ni ufugaji wa nje ambapo kuku huwa na uhuru mkubwa sana wa kutembea wakitafuta chakula wenyewe. Ni kuku wa aina gani wanaweza kufugwa in free range? Aina zote za kuku means 1. Kuku wa kisasa yaani Layers na Broiler 2. Kuku chotara 3. Kuku wa Kienyeji 4. Na aina zingine za kuku. Mahitaji muhumu kwa ajili ya free range. 1. Aridhi ya kutosha/Eneo la kutosha. 2. Miundo mbinu - Maji - Fensi -vivuli -viota vya kutagia. 3. Maji ni kwa jili ya unwagiliaji. 4. Mabanda yao ya kulala. CHAKULA CHAO KINATOKA WAPI? Hapa ndo sehemu huwa watu wanafanya makosa make mtu anaweza waachia kuku wake hata kwenye Lami halafu akasema anawafuga huria. Chakula chao lazima kiandaliwe si kwamba wao ndo waanze kufukuzana na panzi. Kuna aina maalumu ya majani kwa ajili ya freee range na haya ni special kabisa kwa kuku na pia mifugo mingine. Ginger green grass Haya ni...

UBORESHAJI WA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI.

UBORESHAJI WA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI. 1. UTOTOAJI WA VIFARANGA KWA KUTUMIA MAKOO BADALA YA VIATAMIO. Kwa kuwa mfugaji mdogo hawezi kununua mashine ya kuangua mayai, maana ni ghali. Badala yake hutumia kuku wa kienyeji wenye asili ya kuatamia mayai ili wamuangulie vifaranga. Pamoja na kuwa njia hii hutumiwa na wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji, lakini kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi kuhusu ufugaji wa kisasa wa kuku, matokeo yake huw si ya kuridhisha. Tatizo ni mfugaji kushindwa kuwapatia kuku hao mafunzo mazuri. Iwapo kuku wanaoatamia watatunzwa vizuri, kwa mfano, kwa kuwapatia A. Nyumba bora B. Chakula cha ziada C. Maji safi, salama na ya kutosha D. Matibabu ya magonjwa. Kuku hao watafanya kazi zote wao wenyewe. 2. VIOTA KWA AJILI YA KUATAMIA. Badala ya kuacha kuku wajichagulie viota wenyewe ni vizuri zaidi kuwawekea viota karibu na nyumba yako. Hii itafanya wao wenyewe kuwa na sehemu nzuri ya kutaga, hawatokuwa na tabia ya kuham...

Kuku wa nyama broliler wanakua kwa mda wa wiki 4 mpaka kuuzwa wakiwa na kilogram1 pia ukiwapa matunzo mazuri hufikisha mpaka kilo moja na nusu hata zaidi tunaanza na chakula. Wiki mbili za mwanzo hupatiwa broiler starter.

Image
SOMO LA BROLIRER Kuku wa nyama broliler wanakua kwa mda wa wiki 4 mpaka kuuzwa wakiwa na  kilogram1 pia ukiwapa matunzo mazuri hufikisha mpaka kilo moja na nusu hata zaidi tunaanza na chakula. Wiki mbili za mwanzo hupatiwa broiler starter.  Wiki ya tatu hupewa broiler grower . Wiki ya 4 hupewa broiler finisher mpaka kuuzwa ukizingatia ayo hakika watakua vizuri pia mazingira yake yawe ndani sehemu ambayo kuna joto la kutosha  lisio kithiri. Kama  unauwezo weka bulb au hata taa ya chemli kama utashindwa garama za umeme pia kuweka jiko la mkaa kwa ajili ya joto hasa mda wa wiki mbili za mwanzo ni muhimu kwa ajili ya kuwapa joto Kuwa makini kwani joto likizidi  huleta madhara pia.  Chini ya sakafu kunatakiwa pawe na bedding material au kitaalam tunaita litters ila lazima utangulize  magazeti chini ndipo uweke maranda, magazeti hasa  pale wawapo katika siku za mwanzoni , magazeti hukusaidia wewe katika kufanya usafi pale maji yanapo mwagika . Kum...

MAGONJWA ,MATATIZO YANAYOTOKANA NA LISHE DUNI KWA KUKU

Hayo ni.MAGONJWA ,MATATIZO YANAYOTOKANA NA LISHE DUNI Kwa mfano. Kuvimba macho , miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana. Tambua upungufu wa rishe na dalili zake. *UPUNGUFU WA VITAMIN* Upungufu wa vitamin ni uhaba wa vitamin mbali mbali katika mwili wa kuku . DALILI. .Ukungu kwenye macho . Kuku hawakuwi vizuri, wanadumaa manyoya huchelewa kuota. .Vifalanga wadogo kuharisha . Kuku kukonda .Vidole vya miguu kupinda na kuku kushindwa kutembea .Ngozi kuathirika .Ulimi kuvimba .Magamba madogo madogo kuzunguuka mdomo na macho .Miguu kupooza Vifo ni vichache. TIBA: -Tumia vitamin stahiki -Hakikisha unawapatia kuku majani mabichi .mchicha na mboga jamii ya mikunde ; kila mala hasa nyakati za kiangazi. -Changanya vitamin ya dukani kwenye maji. -Hakikisha chakula cha kuku kinakuwa na virutubisho vyenye asili ya wanyama(DCP) - *UPUNGUFU WA MADINI* Upungufu wa madini ni uhaba wa madini kwenye mwili wa ku...

Chakula bora kwa kuku ni mchanganyiko uliozingatia uwiano katika vitu vifuatavyo:

Image
CHAKULA BORA KWA KUKU Chakula bora kwa kuku ni mchanganyiko uliozingatia uwiano katika vitu vifuatavyo: ▶Vyakula vya protini ( protini nyama na protini mimea) hii husaidia katika kujenga mwili na kuunda sehemu zilizoharibika. ▶ Vyakula vya wanga kwa ajili ya kutia nguvu mwili wa kuku. ▶ Madini kama chumvi na chokaa kwa kujenga mifupa na kutengeneza makaka ya mayai. ▶ Mchanga kwa kusaga chakula. ▶Vitamini kwa kutia afya mwili na kumfanya kuu awe mchangamfu ▶ Kazi ya maji katika mwili wa kuku ni kuwezesha chakula hicho kimeng'enywe ili kiweze kuingia mwilini na kufanya kazi iliyokusudiwa. JE KUNA FAIDA GANI YA KUKU KUPEWA CHAKULA BORA Kuku anapopewa chakula bora ▶ Hukua haraka ▶ Hukomaa mapema ▶ Huwa na afya nzuri ▶ Hutaga mayai mengi, makubwa na yenye makaka magumu. ▶ Utagaji wa kuku huendelea kwa kipindi kirefu. ▶ Nyama huwa nyingi, laini na nyeupe. ▶ Uzito wa kuku huongezeka.

SUNGURA... zijue tabia za ufugaji wa sungura

Image
MTAMBUE SUNGURA NA TABIA ZAKE KWA UFUPI Kama ndio unaanza au unataka kuanza kufuga sugura basi haya ni mambo muhimu ya kuyajua Zipo aina nyingi za sungura wa kisasa ambazo zimekuwa zikifugwa na zimethibitika kustahimili mazingira ya kitropiki. Hapa tutaangaalia ana nne ambazo ni rahisi kupatikana. Hizi ni kama ifuatavyo: i. New Zealand: hawa huwa na rangi nyeupe, nyeusi ama nyekundu. Sungura hawa wana macho mekundu. Madume huweza kufikia uzito wa kilo 4.5 na majike kilo 5. Hu fugwa kwa ajili ya nyama. ii. California. Hawa ni weupe lakini pua, masikio, miguu na mikia yao huwa na rangi nyeusi. Wana macho mekundu. Madume huwa na kilo 3.6 hadi 4, na majike 3.9 hadi 4.8. iii. German giant. Wanapatikana katika rangi nyeusi, udongo na kijivu. Wana macho meusi na uzito wa kilo 4-5 lakini katika ufugaji mzuri huweza kufikia hadi kilo sita. iv. Chinchilla. Hawa wapo wa aina tofauti tofauti na uzito wao ni kati ya kilo 3 hadi saba. MIFUMO YA TABIA I. Tabia za ulaji. Sungura kat...

JINSI YA KUTUNZA MAYAI YA KIENYEJI MUDA MREFU

JINSI YA KUTUNZA MAYAI YA KIENYEJI MUDA MREFU Mayai ni kitu ambacho kinaweza kuharibika kwa urahisi kama umakini hautakuwepo hasa kwenye uhifadhi wake. Kwa mayai ya kienyeji soma baadhi a mambo ambayo yatakusaidia kujua namna ya kuhifadhi mayai muda mrefu. Somo hili limelenga uhifadhi wa mayai kwa ajili ya kula au kuuza kwa matumizi ya nyumbani maana mayai kwa ajili ya kuatamishia yana utaratibu wake tofauti wa uhifadhi (somo hili litakuja siku nyingine)  Hakikisha mayai hayana mbegu ya jogoo kwakuwa yai linapokuwa na mbegu ya jogoo then likawekwa kwenye sehemu ya joto maana yake umeliambia yai ANZA KUTENGENEZA KIFARANGA hivyo yai hilo litabadilika na baada ya muda halitafaa kwa kula au kuuza. Ili kuhakikisha mayai yako hayana mbegu ya jogoo fanya yafuatayo: i) Kuwa na banda maalumu kwa ajili ya majike tu bila jogoo hata m1 hii itasaidia mayai yatakayotagwa yasiwe na mbegu ya jogoo. ii) Kama unafuga kwa ajili ya kuuza kwa ajili ya kula na kutotolesha vifaranga hakikish...

UFUGAJI WA SUNGURA...Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda

Image
UFUGAJI BORA WA SUNGURA UTANGULIZI Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama hawa, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu MABANDA Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura. UFUGAJI WA NDANI 1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha 2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa ...

VIDEO....

Image

Jogoo aina hii ya kuchi ukitajiwa bei…. huwezi kuniamini kwa kweli ila nataka uamini anachuana na hata kumzidi ng’ombe…

Image
Jogoo aina hii ya kuchi ukitajiwa bei…. huwezi kuniamini kwa kweli ila nataka uamini anachuana na hata kumzidi ng’ombe… Jogoo la kuchi mdomo kasuku, hatari sana Vifaranga vya kuchi Vikuchi katika ubora wake… kuku watundu sana hawa katika umri huu

KILIMO NA NAMNA YA KULIMA MAINDI...Mahindi ni chakula muhimu na ni aina ya nafaka katika mataifa ya Afrika yaliyomo kusini mwa jangwa la Sahara

Image
UTANGULIZI Mahindi ni chakula muhimu na ni aina ya nafaka katika mataifa ya Afrika yaliyomo kusini mwa jangwa la Sahara. Ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini na kuongeza nguvu mwilini, protini, madini ya chuma (iron) vitamini na madini mengine asilia.Waafrika hutumia mahindi kwa njia mbalimbali (uji, ugali na pombe). Na mahindi ya kuchoma. Kila sehemu ya mmea wa mahindi ina thamani kiuchumi : punje, majani, shina na magunzi huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula na zisizokuwa chakula. Vile vile mahindi ni chakula muhimu cha mifugo (ng’ombe) na huhifadiwa kama silage. Pia mabaki ya mimea na nafaka na pia hutumika viwandani kutengeneza wanga na mafuta. Mahitaji ya mahindi katika hali ya hewa, udongo na Mahindi ni mimea ambayo hustahimili mabadiliko mengi ya hali ya hewa na humea katika maeneo mengi tofauti. Kuna aina nyingi za mahindi yanayotofautiana katika muda wa kukoma...