Chakula bora kwa kuku ni mchanganyiko uliozingatia uwiano katika vitu vifuatavyo:

CHAKULA BORA KWA KUKU
Image result for CHAKULA CHA KUKU
Chakula bora kwa kuku ni mchanganyiko uliozingatia uwiano katika vitu vifuatavyo:
▶Vyakula vya protini ( protini nyama na protini mimea) hii husaidia katika kujenga mwili na kuunda sehemu zilizoharibika.
▶ Vyakula vya wanga kwa ajili ya kutia nguvu mwili wa kuku.
▶ Madini kama chumvi na chokaa kwa kujenga mifupa na kutengeneza makaka ya mayai.
▶ Mchanga kwa kusaga chakula.
▶Vitamini kwa kutia afya mwili na kumfanya kuu awe mchangamfu
▶ Kazi ya maji katika mwili wa kuku ni kuwezesha chakula hicho kimeng'enywe ili kiweze kuingia mwilini na kufanya kazi iliyokusudiwa.
JE KUNA FAIDA GANI YA KUKU KUPEWA CHAKULA BORA
Kuku anapopewa chakula bora
▶ Hukua haraka
▶ Hukomaa mapema
▶ Huwa na afya nzuri
▶ Hutaga mayai mengi, makubwa na yenye makaka magumu.
▶ Utagaji wa kuku huendelea kwa kipindi kirefu.
▶ Nyama huwa nyingi, laini na nyeupe.
▶ Uzito wa kuku huongezeka.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa