hii ndio maana ya ufugaji huria/free range

UFUGAJI HURIA/FREE RANGE
Watu wengi wamekuwa wanauliz kuhusu huu ufugaji wa free range na kutaka kujua ukoje.
Huu ni ufugaji wa nje ambapo kuku huwa na uhuru mkubwa sana wa kutembea wakitafuta chakula wenyewe.
Ni kuku wa aina gani wanaweza kufugwa in free range?
Aina zote za kuku means
1. Kuku wa kisasa yaani Layers na Broiler
2. Kuku chotara
3. Kuku wa Kienyeji
4. Na aina zingine za kuku.
Mahitaji muhumu kwa ajili ya free range.
1. Aridhi ya kutosha/Eneo la kutosha.
2. Miundo mbinu
- Maji
- Fensi
-vivuli
-viota vya kutagia.
3. Maji ni kwa jili ya unwagiliaji.
4. Mabanda yao ya kulala.
CHAKULA CHAO KINATOKA WAPI?
Hapa ndo sehemu huwa watu wanafanya makosa make mtu anaweza waachia kuku wake hata kwenye Lami halafu akasema anawafuga huria.
Chakula chao lazima kiandaliwe si kwamba wao ndo waanze kufukuzana na panzi.
Kuna aina maalumu ya majani kwa ajili ya freee range na haya ni special kabisa kwa kuku na pia mifugo mingine.
Ginger green grass
Haya ni majani maalumu kwa ajili yakupanda kwenye shamba la kuku wako wa free range
Haya majani yanasifa ya kustahimili ukame make hata kama ni kiangazi huwa hayabadiliki rangi au kunyauka
Yanazaliana sana na kwa haraka
Haya majani huwa na virutubisho vifuatavyo.
Sukari huwa ni 14 hadi 15%
Calcium yake ni 1%
Potassimu yake ni 0.5%
Urahisi wa kutafunwa ni ni 84%
Urahisi wa kusagika tumboni ni 75%
Nyuzi nyuzi au fibre 60%
DCP yake(Digestive crude protein) 25%
Pia unaweza otesha majani kama vile.
Lusina,
Wadudu ni muhimu na watapatikana kupitia kufanya umwagiliaji wa shamba lako.
ENEO LINALO HITAJIKA.
Inategemeana ila mara nyingi tunashauriwa kuku 1000 hadi 2000 kwa heka 1.
MUDA WA KUKAA NJE
Mara nyingi ni masaa 8 hadi 12 yaani asubuhi hadi jioni saa 11 au 12 na baada ya hapo kuku wanarudishwa ndani kulala.
VIOTA VYAO.
Hawa kuku wanaweza jengewa viota vyao huko huko nje kwenye majani na wakawa wanatagia huko huko na kazi ikawa ni kuokota.
WAKATI WA MVUA
Huwa inashauriwa kuwe na vivuri vya kutosha na hata hivyo hawa kuku wanaweza kaa kwenye mvua hawana shida ila wakati wa mvua kubwa kuwe na vyumba vya kujikinga au wanaweza rudishwa bandani
MAYAI YAO
Mayai ya free range ni ya daraja la kwanza na kamwe sio mayai ya kwenda kukaangia chips bali ni mayai yanayo takiwa kuuzwa sehemu maalumu na kwa watu maalumu.
Fertilized eggs
Huwa haifai kufuga kuku wazazi free range, itakuwa ni kazi ngumu na pia mayai yao yanaweza pata shida so free range ni kwa mayai ya kula sana na kuku wa kula
Faida za free range.
Unaingia gharama chache hasa kwenye vyakula
Mayai yenye ubora wa hari ya juu kabisa.
Kuku pia wanakuwa hawapati maradhi sana.
Hasara zake
Kuku kukamatwa na wanyama na ndege, inahitajika eneo na pia fensi ni muhimu sana msije gombana na jirani yako.
NB: Ni ufugaji mzuri sana endapo una miundo mbinu

Comments