JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA WEWE MWENYEWE.

JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA WEWE MWENYEWE.
Vyakula vya kuku huweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe.
Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa
Chakula hicho lazima kiwe na chakula hicho lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile wanga, protini, madini na vitamini.
Hakikisha chakula unachotengeneza wewe kiwe na mchanganyiko wa vyakula ifuatavyo:

▶ Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, pumba, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti.
▶ Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, mchicha majani ya mpapai na nyasi mbichi.
▶ Vyakula vya kujenga mifupa kama vile aina ya madini chokaa mifupa iliyosagwa na chumvi.
Ukosefu wa vitamini na madini kama kalsiamu na fosforasi husababisha kuku kuwa na matege, vidole kukunjamana. Misuli kufyatuka na kupofuka macho.
▶ Maji ni muhimu sana kwani husaidia kulainisha na kurahisisha usagaji wa chakula na kupunguza joto kali.
Wakati wa joto kali kuku wapewe maji mengi.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa