SUNGURA... zijue tabia za ufugaji wa sungura
MTAMBUE SUNGURA NA TABIA ZAKE KWA UFUPI
Kama ndio unaanza au unataka kuanza kufuga sugura basi haya ni mambo muhimu ya kuyajua Zipo aina nyingi za sungura wa kisasa ambazo zimekuwa zikifugwa na zimethibitika kustahimili mazingira ya kitropiki. Hapa tutaangaalia ana nne ambazo ni rahisi kupatikana. Hizi ni kama ifuatavyo:
i. New Zealand: hawa huwa na rangi nyeupe, nyeusi ama nyekundu. Sungura hawa wana macho mekundu. Madume huweza kufikia uzito wa kilo 4.5 na majike kilo 5. Hufugwa kwa ajili ya nyama.
ii. California. Hawa ni weupe lakini pua, masikio, miguu na mikia yao huwa na rangi nyeusi. Wana macho mekundu. Madume huwa na kilo 3.6 hadi 4, na majike 3.9 hadi 4.8.
iii. German giant. Wanapatikana katika rangi nyeusi, udongo na kijivu. Wana macho meusi na uzito wa kilo 4-5 lakini katika ufugaji mzuri huweza kufikia hadi kilo sita.
iv. Chinchilla. Hawa wapo wa aina tofauti tofauti na uzito wao ni kati ya kilo 3 hadi saba.
MIFUMO YA TABIA
I. Tabia za ulaji. Sungura katika mfumo wao wa ulaji wametengenezwa kukubaliana na ulaji wa majani ikiwa ni pamoja na kuwa na tumbo
kbwa la nyuma. Hata hivyo sungura hubagua vyakula katika ulaji wao, hupendelea majani kuliko mashina, mimea michanga kuliko iliyo komaa, na majani mabichi kuliko makavu. Wanapokuwa wakila huinua vichwa kutazama mazingira kama ni salama.
II. Tabia za kijinsia. Hapa mara nyingi jike hupelekwa katika banda la dume na ndani ya muda mfupi hupandwa. Jike hupelekwa kwa dume kuliko dume kupelekwa kwa jike kwa sababu ya tabia ya upandaji wa kimipaka hivyo zoezi hufanyika haraka. Kama dume likipanda kwa mafanikio miguu ya nyuma huinuka na kuangukia nyuma au pembeni baada ya kutoa mlio. Shauku ya dume kupanda huendeshwa na homoni na shauku hii ni moja ya vigezo unapochagua dume la kutumia. Ikumbukwe sungura jike hana muda maalum wa kuingia kwenye joto bali anapowekwa tu na dume joto huja ndani ya muda mfupi na hii huitwa AUTOMATIC HEAT.
III. Tabia za uzazi. Kwa kawaida sungura huchagua eneo la kuzalia siku kadhaa kabla ya kuzaa, huliandaa eneo na mwisho huzaa na kuwatunza watoto wake. Wiki moja kabla ya kuzaa sungura kuanza kubeba majani laini katika mdogo wake kuanda eneo la kuzalia. Siku moja kabla ya kuzaa sungura hujinyonyoa manyoya yake mwenyewe kuandaa eneo la kuzalia. Baada ya kuzaa sungura hula mabaki ya uzazi na uteute wake jambo ambalo husaidia kuepusha maambukizi ya bacteria kwa watoto wake na pia huondoa harufu ambayo huvutia wanyama hatari. Sungura hubeba mimba kwa siku 30 (wastani). Na katika utunzaji mzuri huzaa hadi mara sita kwa mwaka kwa wastani wa watoto nane hadi kumi kwa uzao mmoja.
Hizi ni baadhi tu ya tabia za sungura ambazo tumeona ni muhimu uzifahamu hata kabla hujaanza kufuga sungura.
*kwa hayo machache yatakupa mwanga mzuri kwenye ufugaji wako wa sungura cha ila kuna jambo moja na sisitiza kama unataka wazaliane wawe wengi usiwalishe saaana wakinenepa sana uzazi unakuwa taabu wape msosi saizi yakati tu

Comments
Post a Comment