ASALI NA FAIDA ZAKE:
ASALI NA FAIDA ZAKE: Asali kama chakula na pia dawa ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu. Kwa mfano yapata miaka 4,000 (elfu nne) iliyopita madakatari wa tiba wa Kimisri na wale wa Sumarani waliitumia asali kutibu magonjwa mbali mbali kama vile vidonda vya tumbo na vile vya kawaida, magonjwa ya macho, ngozi na yale ya tumbo. Historia pia imerikodi matumizi kama hayo kwa watu wa Uchina, Ugiriki, Roma, n.k. Hippocrates, baba wa tiba kwa nchi za magharibi pia alitumia asali kutibu magonjwa mbali mbali, vile vile Ibn Sina, mfalme wa tiba kutoka katika ulimwengu wa nchi za Kiislamu ameorodhesha faida nyingi za matumizi ya asali, katika buku lake la tiba maarufu "The Canon of Medicine". Miongoni mwa faida alizotaja Ibn Sina katika buku hilo (Misingi ya tiba) ni kuweka mwili katika hali ya ujana, kuongeza uwezo wa kukumbuka mambo, kuleta furaha, kusaidia usagaji wa chakula kuongeza hamu ya kula chakula, na kuongeza uwezo wa mtu kuzungumza vizuri. Elimu ya Sayansi (y...