TUMIA KAROTI KAMA TIBA

Karoti pamoja na kuwa na faida nyingi mwilini ikiwa utakula walau karoti si chini ya sita kwa wiki au moja kwa siku iwe unakula kwa kuzichemsha, mbichi, kuweka kwenye salad, kutengeneza juice na smoothie, supu, kutafuna nk.
Karoti hupatikana kwa wingi sokoni na magengeni japokuwa wengi wetu huwa tunaziona tu na hata wengine tunazinunua na kuishia kuzila kwenye michuzi ya nyama na vyakula vingine, Bei yake huwa ya kawaida sana kulingana na hali ya vipato vyetu lakini huwa na faida nyingi muhimu kwa afya zetu. Zinatupa manufaa mengi kuliko gharama kama inavyoelezwa hapo chini;

1) karoti husaidia kuimarisha macho kuona vizuri, mfano tatizo la kutoona vizuri usiku, pia inasaidia kuondoa matatizo ya allergy kwenye macho mfano macho kuwasha sababu ya vumbi.
karoti inarutubisha cells mwilini na kuzifanya zisizeeke haraka. Hii inatokana na uwepo wa Vitamin A ambayo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa macho kuona.
2)Huifanya ngozi iwe nzuri na yenye afya, kama utatumia kurutubisha ngozi yako, ikwangue kwa kutumia grater kiasi unachotaka tia asali mbichi kijiko 1 kikubwa (cha kulia chakula) mafuta ya nazi au olive kijiko kimoja kikubwa na limao kijiko 1 kikubwa changanya vizuri, kisha itumie kusugua mwilini sehemu yoyote unayotaka, ukimaliza acha kama dakika 15 na zaidi kisha oga, itasaidia kuondoa taka katika vinyweleo, kuifanya ngozi iwe laini na kuondoa mikunjo katika ngozi. KUMBUKA INATAKIWAASALI MBICHI, SIYO ASALI YOYOTE, IKIWA UNAHITAJI ASALI MBICHI WASILIANA NASI 0719163972 TUTAKUTUMIA POPOTE ULIPO.
-Karoti husaidia kuondoa sumu na taka mwilini, inaondoa mafuta yasiyotakiwa katika ini (Cholesterol) na kuliwezesha lifanye kazi vizuri, kusafisha njia ya haja kubwa na kusaidia kupata choo vizuri (kuzuia constipation).
3)Karoti zinasaidia kufanya fizi na meno kuwa imara na kuchochea uzalishwaji wa mate.
-Pia inasaidia kuzuia stroke(Kiharusi), Watafiti wa Harvard University wamegundua kuwa watu wanaokula karoti walau sita kwa wiki wana uwezekano mdogo wa kupata stroke. Pia
Wamegundua karoti zinatibu tatizo la kupoteza kumbukumbu kwa wazee.
4) karoti hupunguza hatari ya kupata SHINIKIZO LA DAMU (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (blood vessels) na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).
5)karoti pia husaidia kuzuia magonjwa mengine kama vile Kisukari (Diabetes),Kiharusi (Stroke), kansa pamoja na magonjwa ya moyo.


6)Zaidi husaidia kuongeza kinga mwilini (immune booster).. hii hutokana na tabia asilia ya karoti kuwa na antibacteria pamoja na antiseptic ambazo husaidia kuzuia kinga za mwili. Pia Karoti ina vitamin C muhimu kwa kusisimua seli nyeupe za damu (white blood cells) ambazo ni sehemu muhimu katika kinga ya mwili.

Comments