ASALI NA FAIDA ZAKE:
Asali kama chakula na pia dawa ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu. Kwa mfano yapata miaka 4,000 (elfu nne) iliyopita madakatari wa tiba wa Kimisri na wale wa Sumarani waliitumia asali kutibu magonjwa mbali mbali kama vile vidonda vya tumbo na vile vya kawaida, magonjwa ya macho, ngozi na yale ya tumbo. Historia pia imerikodi matumizi kama hayo kwa watu wa Uchina, Ugiriki, Roma, n.k. Hippocrates, baba wa tiba kwa nchi za
magharibi pia alitumia asali kutibu magonjwa mbali mbali, vile vile Ibn Sina, mfalme wa tiba kutoka katika ulimwengu wa nchi za Kiislamu ameorodhesha faida nyingi za matumizi ya asali, katika buku lake la tiba maarufu "The Canon of Medicine". Miongoni mwa faida alizotaja Ibn Sina katika buku hilo (Misingi ya tiba) ni kuweka mwili katika hali ya ujana, kuongeza uwezo wa kukumbuka mambo, kuleta furaha, kusaidia usagaji wa chakula kuongeza hamu ya kula chakula, na kuongeza uwezo wa mtu kuzungumza vizuri. Elimu ya Sayansi (ya kisasa) nayo
imemwezesha mwanadamu kufahamu kwa kina ubora wa asali. Kwa mfano, tangu mwaka 1937 wanasayansi walijua kwamba wingi wa sukari iliyomo katika asali (76gllooml), tindikali (acidity, Ph = 3.6-4.2), na kuwemo kwa baadhi ya kemikali zinazotokana na viumbe hai (Organic
Compounds).
Ni sababu zinazoifanya asali kuwa ni dawa. Yaani inaweza kuulinda mwili usipate maradhi na pia inaweza kuviua vijidudu vya maradhi vilivyomo ndani ya mwili wa mgonjwa. Zaidi ya hayo, sayansi inatujulisha kuwa, asali inamchanganyiko wa virutubisho na kemikali za aina mbali mbali. Baadhi ya vitu hivyo ni sukari, vitamini, amino acids (vitu vinavyotengeneza protini), vimeng'enyo (enzymes), homeni (hormones). (Sura ya 16, "An-Nahl"). Moja ya aya
inayopatikana katika sura hiyo inayomwelezea kiumbe nyuki na teknolojia yake kongwe ya utengenezaji wa asali ni hii: (16:68). Namalizia makala hii kwa kuwahimiza wananchi wazidishe siyo tu uzalishaji bali pia matumizi ya asali ili kujenga afya zetu na uchumi wetu.
Kwa maitaji yako ya asali hii ambayo zipo za aina mbili
1. Iliyokuwa bado ikiwa na masega yake pamoja na vitu vyote ni kutokana na watu wengi wanapenda asali katika mfumo huu kwa ajiri ya kujiahakikishia kuwa asali yao ni salama kabisa na haijachakachuliwa
2. Zinapatikana asali amazo zimechunjwaa kwa utaaramu wa makini kabisa hili iweze kumfikia mteja wetu nae aweze kufurahia bidhaa yake
3. Ikiwa upo ofisini nyumbani na ukaitaji asali na huna muda wa kuanza kuitafuta au kununua sisi tunakuletea hapo ulipo
4. Wasiliana nasi
+255 719163972, 0687899064
Comments
Post a Comment