MAFUTA YA HABBAT SAWDA NA KAZI YAKE
MATUMIZI ya mafuta ya habat soda ni mengi sana katika mwili wa binadamu lakini leo utajifunza na kufaidika na haya machache ambayo ninayaandika hapa chini: KWA AFYA Kunywa kijiko kimoja cha mafuta haya asubuhi na usiku, tena asubuhi unaweza kunywa kabla ya kifungua kinywa. Unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi. HAMU YA KULA Kabla ya kuanza kula, jipatie kijiko kimoja cha mafuta hayo kisha kunywa maji ya kawaida au yaliyochanganywa na siki kidogo.
VIPELE, CHUNUSI NA NGOZI Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha habat soda iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tufaha (apple). Paka sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko huu unaweza kukaa mpaka wiki tatu, ni lazima uuweke katika hali ya baridi.
PUMU Weka kijiko cha habat soda iliyochemshwa katika maji yaliyochemshwa kisha unywe ikiwa ya moto.
KUTIBU MGONGO (sehemu ya chini) Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha habat soda kunywa kabla hujala kitu chochote wakati wa asubuhi.
KIBOFU/FIGO Kama unasumbuliwa na kibofu cha mkojo au figo, tumia asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya habat soda iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi. Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko huu pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko wa asali na habat soda unaweza kukaa kwa siku 15 tu na hifadhi kwenye baridi.
KIKOHOZI Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya habat soda kwenye kahawa au chai. Kunywa kijiko kimoja cha habat soda na asali mchana na usiku. Pia kwa wenye matatizo ya kutokwa na haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha habat soda pamoja na asali, kisha kunywa maji ya uvuguvugu.
NGOZI KAVU Kwa wale wenye ngozi kavu changanya asali pamoja na robo kijiko cha mafuta ya habat soda, kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
MINYOO: Kunywa habat soda pamoja na siki kuondoa minyoo ya aina yoyote ile, inaweza kuwa ya limao au ya tufaha ‘apple’
. KICHWA Kama unasumbuliwa na kichwa, chukua unga wa habat soda, karafuu iliyosagwa nusu, kijiko cha habat sauda kisha uchanganye. chukua kijiko kimoja cha chai kisha kunywa na mafuta yake unaweza kupaka kichwani.
USINGIZI Kama una tatizo la kukosa usingizi, chukua kijiko kimoja cha habat soda changanya na maziwa glasi moja pamoja na asali kijiko kimoja kikubwa kisha kunywa.
SIKIO Chukua tone moja la mafuta ya habat soda nyunyizia ndani ya sikio husaidia kulisafisha na kuliponya kabisa.
MALENGELENGE Chukua mafuta ya habat soda jipake mpaka yaishe.
MARADHI YA WANAWAKE Tumia mafuta ya habat soda, kunywa kwenye kila kinywaji cha moto, unaweza kuweka kijiko kimoja kwenye maziwa, kwenye maji ya moto, kwenye supu n.k. Mbali na matatizo hayo pia inasaidia kusafisha kizazi na ni rahisi kwa mwanamke asiyezaa kushika mimba kwa haraka.
KUSIKIA VIZURI Mtu mwenye ugonjwa wa kutosikia achemshe habat soda na karafuu, anywe bila kuongeza kitu chochote mara tatu kwa siku atapona.
VIDONDA Kama una kidonda changanya matone kumi ya mafuta ya habat soda katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Kula mchanganyiko huu kabla ya kula chakula baadaye kunywa glasi ya maziwa yasiyotiwa kitu chochote.
Comments
Post a Comment