Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote
Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote MTI WA MBILIMBI (M-MBILIMBI) Huu ni mmea unaopatikana sana sehemu za pwani kama Zanzibar, Tanga, Dar es salaam, Kibaha n.k Ni mmea ambao hauwezi kuhimili ukame wala baridi kali na unastawi zaidi kwenye mvua za kutosha na udongo usiotuamisha maji kabisa. MATUMIZI Miaka mingi mbilimbi zimekuwa zikijulikana kwa matumizi ya achali ndio maana sehemu nyingine mbilimbi zilitungwa jina la PICKLE FRUIT. Utengenezaji wa achali uko wa kuchanganya vitu tofauti tofauti kama nyanya, vitunguu, pilipili, ndimu, malimao, chumvi, maembe n.k ambavyo vinankuwa katika vipande vidogo vidigo, unaweka kwenye chupa na kuanika juani kwa siku kadhaa (ingawa baadhi huupika mchanganyiko huu) Mbilimbi pia hutumika kutengenezea siki (vinegar) na mvinyo, hii mara nyingi hufanyika viwandani na sio majumbani kama ilivyo achali. Mbilimbi pia ni dawa kwa magonjwa kama chunusi, kifua na kukohoa na mengineyo mengi. Ili kutibu kukohoa unatakiwa utafune mbilimbi kama ...
Good
ReplyDelete