Posts

Showing posts from March, 2017

VIDEO: biogas

Image

MUHIMU: ujue mtambo wa biogas

Image
Utangulizi Bayogesi (biogas) ni kitu gani? Bayogesi ni mchanganyiko wa gesi inayoundwa na viasilia mbalimbali vinavyotengenezwa katika mazingira ya kutokuwepo hewa (oksijeni) ambayo asilimia kubwa ni gesi ya methane (CH 4 ). Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea mitambo mbalimbali. Matumizi ya gesi hii kwa mtu ambaye ana mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe yanaweza kusaidia kuondokana na gharama za kununua nishati ya kuni, mkaa, umeme na hata gesi asilia inayochimbwa ardhini. Gesi hii inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo vingine vya nishati. Mfano, gharama za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji atakayedhamiria kutumia jiko la um eme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya samadi mtumiaji itamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa hana malipo ya pesa kila mwezi kama it...

MAELEKEO:soma maelekezo ya mtambo wa biogesi

Image
MAELEZO ZAIDI YA MITAMBO YA BIOGESI MUHIMU :Unaweza kuchagua ukubwa wa mtambo wa nishati ya gesi kutegemea idadi ya mifugo uliyonayo na mahitaji yako ya nishati. Ukubwa wa Mtambo Idadi ya Ng’ombe Masaa ya kupika kwa siku: Ukubwa wa Mtambo Idadi ya Ng’ombe Masaa ya kupika kwa siku 4m3 2 → 3 2→ 4 6m3 4→ 5 4→ 6 9m3 5→ 7 6→ 10 13m3 10→15 8→15 Idadi iliyoonyeshwa ni ya ng’ombe wanaolishwa kwenye zizi muda wote ambapo kinyesi hupatikana kutoka kwenye zizi.  Kama ng’ombe hupelekwa malishoni wakati wa mchana na kurudi kwenye zizi wakati wa usiku, inatakiwa kupatikana kinyesi sawa na ng’ombe wasio chungwa ili kupata kiasi cha gesi kinacholingana na mahitaji yako.  JE, UNAHITAJI NINI KUWA NA MTAMBO WA NISHATI YA GESI? 1) Unahitaji kuwa na angalau ng’ombe wawili wa kudumu karibu na mtambo.  2) Ng’ombe wako wawepo ...

UFUGAJI: NJIA YA KUJUA KUWA KUKU WAKO ANA UGONJWA WA TYPHOD, KINGA NA TIBA ZAKE

Image
UGONJWA WA HOMA YA MATUMBO ( TYPHOID) Huu ni ugonjwa hatari unaouwa vifaranga na kuku wakubwa pia. Huambukiza kuku na bata mzinga pia. Kama ilivyo kwa binadamu, ugonjwa huu husababishwa na bakteria na huambukiza kupitia yai au vyakula na maji vilivyochafuliwa na kinyesi au damu kutoka kwa ndege wenye maambukizi ya ugonjwa huu. Ugonjwa huu huonekana kama magonjwa mawili. Kwanza hushika vifaranga au kuku ambao hawajakua sana na huchangiwa zaidi na uchafu wa kwenye mabanda. Pi li huwakumba wale kuku wakubwa. UENEZAJI... A. Ugonjwa huu huweza kuenezwa kutoka kwa makoo yaliyo na ugonjwa huu kupitia mayai kwenda kwa kifaranga. B. Ni vigumu kuudhibiti ugonjwa huu katika mabanda ambayo hayana sakafu ya saruji. C. Tabia ya kuku kudonoana hueneza pia ugonjwa huu. Bakteria humuingia kifaranga au kuku kupitia vidonda vilivyosababisha na kudonoana. D. Mayai yaliyoambukiza na ugonjwa huu yakiliwa na binadamu hudhuru afya zao pia. DALILI ZA UGONJWA HUU.... A. KWA VIFARANGA...

UFUGAJI: JUA NJIA ZA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI.

Image
UBORESHAJI WA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI. 1. UTOTOAJI WA VIFARANGA KWA KUTUMIA MAKOO BADALA YA VIATAMIO. Kwa kuwa mfugaji mdogo hawezi kununua mashine ya kuangua mayai, maana ni ghali. Badala yake hutumia kuku wa kienyeji wenye asili ya kuatamia mayai ili wamuangulie vifaranga. Pamoja na kuwa njia hii hutumiwa na wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji, lakini kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi kuhusu ufugaji wa kisasa wa kuku, matokeo yake huw si ya kuridhisha. Tatizo ni mfugaji kushindwa kuwapatia kuku hao mafunzo mazuri. Iwapo kuku wanaoatamia watatunzwa vizuri, kwa mfano, kwa kuwapatia A. Nyumba bora B. Chakula cha ziada C. Maji safi, salama na ya kutosha D. Matibabu ya magonjwa. Kuku hao watafanya kazi zote wao wenyewe. 2. VIOTA KWA AJILI YA KUATAMIA. Badala ya kuacha kuku wajichagulie viota wenyewe ni vizuri zaidi kuwawekea viota karibu na nyumba yako. Hii itafanya wao wenyewe kuwa na sehemu nzuri ya kutaga, hawatokuwa na tabia ya kuhamaha...

njia za kulea vifaranga kwa siku 1 mpaka wiki 5

Image
KULEA VIFARANGA (SIKU 1 HADI WIKI 5). MAANDALIZI KABLA NA MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA. A. MAANDALIZI KABLA YA KUPOKEA VIFARANGA. Inashauriwa vifaranga walelewe katika chumba maalum hadi umri wa majuma manne. Chumba kitayarishwe siku kumi na nne kabla ya vifaranga kuwasili kama ifuatavyo: >Matundu yote yaliyo kwenye sakafu, dari, madirisha na ukuta yazibwe. >Kama chumba hicho kina sakafu ya saruji, kisafi shwe kwa maji ya moto na baadaye kinyunyizie dawa kama vile Rhino au Dettol ya kuua wadudu. Ikiwa chumba hicho hakina sakafu ya saruji, toa takataka zote kisha mwagia chokaa au majivu. >Mazingira ya nje ya banda yawekwe katika hali ya usafi ili kuzuia wadudu waharibifu. Kusafi shwe hadi kufi kia upana wa mita mbili au zaidi kuzunguka banda. >Katika chumba watakamofikia vifaranga tengeneza sehemu maalum ya kulelea (kitalu). Sehemu hiyo maalum inatakiwa iwe na umbile la duara, itengenezwe kwa kutumia karatasi ngumu au majamvi. Mduara huhifadh...

hile kampuni ya THE RABBIT BLISS kwa wafugaji sungura sasa hipo dar es salaam

Image
KAMPUNI YA KUFUGA SUNGURA YA "THE RABBIT BLISS" SASA YAHAMIA JIJINI DAR  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben akizngumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii alietembelea makao makuu mapya ya Kampuni hiyo, yaliyopo eneo la Majohe, jijini Dar es salaam. Kampuni hiyo hivi sasa ipo Dar es salaam ikitokea Jijini Arusha kulikokuwa na makazi yake ya awali baada ya mmiliki wa sasa kununua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na mmiliki wa awali. Akizungumza katika eneo hilo, Bw. Ruben alisema kuwa ufugaji wa Sungura ni mzuri sana na unafaida kubwa kwa mfugaji, kwani unaweza kumuingia kipato kikubwa kama atazingitia taratibu zote za ufugani, hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kufuga au kujifunza ufugaji wa Sungura wasisite kufika kwenye ofisi zao zilizopo Majohe, Jijini Dar es salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufu...

Ufugaji: fata njia hizi uweze kufanikiwa kwenye ufugaji wa kuku

Image
1.      banda la kuku o    Vifaa vinavyotumika kwa ujenzi wa banda o     ukubwa wa banda 2.      Eneo linalohitajika kufuga kuku kwenye 3.      Sakafu ya matandazo kutegemea na umri na aina ya kuku 4.      Vifaa na vyombo muhimu 5.       uchaguzi wa kuku bora wa kufuga 6.       kuku wa asili 7.      Masuala ya kuzingatia wakati wa kumchagua kuku 8.      Mtagaji asili 9.       kuku wa kisasa 10.                         kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa 11.                      ...

UFUGAJI WA KISASA NI UWEKEZAJI WENYE TIJA.

UFUGAJI WA KISASA NI UWEKEZAJI WENYE TIJA. Ufugaji wa kisasa ni moja ya mambo yanayoweza kumpatia mkulima na hata mtu mwingine kipato cha ziada akiamua kuwekeza huko. Kama dhana ya uwekezaji inavyomaanisha kuwa ni shughuli ambayo huweza kumpatia mtu kipato bila kuathiri muda wake wala kazi nyingine anayofanya. Hata kwa wale walioajiriwa wanaweza kufanya pia ufugaji wa aina hii na kujiingizia kipato cha ziada mbali na kile kipato chao kingine, sema japo la kuzingatia kwako ni usimamizi wa kuweza kuangalia mifugo hiyo kwa karibu zaidi. Tunapozungumzia ufugaji wa kisasa ni ule ufugaji mkubwa na wenye tija na wenye lengo la kibiashara ukiachilia mbali ule wa mazoea. Mradi wa ufugaji unahitaji mtaji utakaomwezesha mtu kuandaa mazingira mazuri ya kuhifadhia mifugo pia kutafuta aina nzuri ya mifugo anayotaka mfugaji huyu nk Mfano unapoamua kufuga kuku wa mayai wa 500 au wa nyama 500. Huu ni mradi mkubwa ambao baada ya muda mfupi faida huanza kuonekana, kama tujuavyo kuk...

kilio cha vitunguu

Image
Vitunguu ni moja ya zao la bustani linalopendwa na kutumiwa kwa wingi sana si hapa nchini tu bali duniani kote kwa ujumla. Linachukua nafasi ya pili baada ya nyanya. Kitunguu kinatumika katika kachumbari, kama kiungo kwenye kitoweo kama vile Samaki, nyama, mboga za mahani n.k. Majani ya vitunguu hutumika kama mboga. Vitnguu pia hutumika kuandalia supu. Vitunguu hustawi maeneo yasiyo na mvua nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na maeneo yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa kwa vitunguu. Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha, unaoruhusu mizizi kupenya na unaohifadhi unyevu kama vile udongo wa nusu mfinyanzi nusu tifutifu. UPANDAJI WA MBEGU ZA VITUNGUU KWENYE KITALU. Hapa kwetu Tanzania upandaji huanza mwezi March hadi Mei kutegemea na msimu wa kilimo ulivyo. Hivyo kilimo hiki huanza mara baada ya mvua kubwa za masika kumalizika. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri wa vit...