UFUGAJI WA KISASA NI UWEKEZAJI WENYE TIJA.



UFUGAJI WA KISASA NI UWEKEZAJI WENYE TIJA.
Ufugaji wa kisasa ni moja ya mambo yanayoweza kumpatia mkulima na hata mtu mwingine kipato cha ziada akiamua kuwekeza huko. Kama dhana ya uwekezaji inavyomaanisha kuwa ni shughuli ambayo huweza kumpatia mtu kipato bila kuathiri muda wake wala kazi nyingine anayofanya.
Hata kwa wale walioajiriwa wanaweza kufanya pia ufugaji wa aina hii na kujiingizia kipato cha ziada mbali na kile kipato chao kingine, sema japo la kuzingatia kwako ni usimamizi wa kuweza kuangalia mifugo hiyo kwa karibu zaidi.
Tunapozungumzia ufugaji wa kisasa ni ule ufugaji mkubwa na wenye tija na wenye lengo la kibiashara ukiachilia mbali ule wa mazoea.
Mradi wa ufugaji unahitaji mtaji utakaomwezesha mtu kuandaa mazingira mazuri ya kuhifadhia mifugo pia kutafuta aina nzuri ya mifugo anayotaka mfugaji huyu nk
Mfano unapoamua kufuga kuku wa mayai wa 500 au wa nyama 500. Huu ni mradi mkubwa ambao baada ya muda mfupi faida huanza kuonekana, kama tujuavyo kuku wa kisasa wanazalisha mayai mengi kwa muda mfupi.
Soko la mayai pia huwa ni la uhakika hasa katika maeneo ya mjini, kwa hiyo inahitaji usimamizi mzuri wa mradi ili uweze kujiingizia kipato kikubwa kwa hapo baadaye kitakachokuwezesha kutimiza mahitaji yako mengineyo na si kutegemea mshahara tu.
Changamoto kubwa kwa watu wengi katika ufugaji Huu wa kisasa ni uthubutu katika kufanya maamuzi hasa kwa jambo ambalo hujawahi kulifanya. Kuna wanyama wengi wana faida endapo watafugwa kibiashara.
Kabla hujawekeza katika mradi huu lazima ujiridhishe kwanza juu ya upatikanaji wa soko la bidhaa zako. Kama ni nyama, mayai, damu, ngozi au mbolea. Unapoona soko la uhakika yalipo, lazima ufikirie ni jinsi gani utawezaje kuwafanya watu waipende bidhaa yako.
Unapopata uhakika wa hilo, basi huna budi kuanza mradi wako na kuusimamia vyema ili usiweze kupata hasara kabla ya mavuno.
Mara nyingi mwanzo huwa na changamoto nyingi, lakini jambo muhimu ni uvumilivu na kujua nini cha kufanya katika kukabiliana na changamoto hizo. Changamoto kubwa huwa ni kuandaa miundombinu ya kufugia.
Baada ya kukamilika kwa miundombinu, mfugaji unatakiwa kuchagua aina bora ya mifugo. Kuna aina nyingi na makabila mengi ya mifugo kwa hiyo Wewe kama mfugaji lazima uangalie ni aina gani ya mifugo unaofaa kibiashara.
Faida ya kuwa na aina bora ya mifugo ni kuongeza thamani ya mazao sokoni, kama ni mifugo wenyewe, nyama, ngozi au mazao mengine yanayotokana na mifugo hiyo. Ni muhimu kuzingatia kuwa bidhaa bora ndiyo inafanya vizuri sokoni.
Ili kuwa na uthubutu katika kuhakikisha aina hii ya uwekezaji, mfugaji unatakiwa kuwa na mambo muhimu matatu.
1. MTAJI WA KUTOSHA. Mtaji wa kutosha ambao utakufanya uweze kuwahudumia mifugo wako kabla hujaanza kuiona faida.
Ni muhimu kufanya hivyo kwani unapofuga Bila kuzingatia hiki ndiyo mwisho wa siku mtu anakumbwa na matatizo mengine anajikuta anaamua kuuza mifugo yake ikiwa bado midogo na pia wengine kukaa tamaa kabisa.
2. USIMAMIZI MZURI WA MRADI. Wanyama ni kama watoto, wanahitaji kuangaliwa mara kwa mara na kutibiwa pale wanapoonyesha dalili za ugonjwa. Unaweza kutumia muda wako au kuwaajili watu wa kuweza kuangalia mifugo wakati unapokuwa haupo.
3. ENEO LA KUTOSHA. Kuwa na eneo la kutosha kwa ajili ya mifugo. Ufugaji mkubwa wa kibiashara unahitaji eneo kubwa ambalo litaruhusu mifugo kukaa vyema.
Usafi wa mabanda lazima uzingatiwe ili kuweza kuwakinga kuku na magonjwa mbalimbali

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa