njia za kulea vifaranga kwa siku 1 mpaka wiki 5

KULEA VIFARANGA (SIKU 1 HADI WIKI 5).
MAANDALIZI KABLA NA MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.
A. MAANDALIZI KABLA YA KUPOKEA VIFARANGA.
Inashauriwa vifaranga walelewe katika chumba maalum hadi umri wa majuma manne. Chumba kitayarishwe siku kumi na nne kabla ya vifaranga kuwasili kama ifuatavyo:
>Matundu yote yaliyo kwenye sakafu, dari, madirisha na ukuta yazibwe.
>Kama chumba hicho kina sakafu ya saruji, kisafi shwe kwa maji ya moto na baadaye kinyunyizie dawa kama vile Rhino au Dettol ya kuua wadudu. Ikiwa chumba hicho hakina sakafu ya saruji, toa takataka zote kisha mwagia chokaa au majivu.
>Mazingira ya nje ya banda yawekwe katika hali ya usafi ili kuzuia wadudu waharibifu. Kusafi shwe hadi kufi kia upana wa mita mbili au zaidi kuzunguka banda.
>Katika chumba watakamofikia vifaranga tengeneza sehemu maalum ya kulelea (kitalu). Sehemu hiyo maalum inatakiwa iwe na umbile la duara, itengenezwe kwa kutumia karatasi ngumu au majamvi. Mduara huhifadhi joto, huzuia upepo na huzuia
vifaranga wasiende mbali na chanzo cha joto.
>Sakafu iwekwe matandazo yaliyopigwa dawa mfano ya kuuwa wadudu kama Municipal disinfectant. Matandazo yaweza kuwa pumba ya mpunga, maranda ya mbao, nyasi, mchanga, maganda ya karanga n.k. Masaa mawili kabla ya kuwasili vifaranga vyenye umri wa siku moja taa au jiko liwashwe kwenye chumba cha kulelea vifaranga. Hii itasaidia ili maji na chumba kuanza kupata joto la
kutosha kuwawezesha vifaranga kula, kunywa bila shida.
>Baada ya masaa mawili kupita ndipo chakula kianze kuwekwa kwenye vyombo vya chakula na vifaranga waanze kula.
B. MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.
∆ Kuwapa joto.
Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia Kitalu (mduara) unaoweza kutengenezwa kwa kutumia mbao au karatasi ngumu. Au kwenye pembe moja ya chumba ambapo utawaweka vifaranga zungusha vifaa vya kutunza na kuongeza joto . Vifaranga hujikusanya karibu nachanzo cha joto kama taa au jiko kujilundika katika sehemu moja kama joto ni kidogo. Hivyo ongeza joto kwa kushusha taa chini na kama bado joto litakuwa halitoshi, ongeza vifaa vya joto kama taa ya pili kutegemeana na hali halisi.
KAMA JOTO HALITOSHELEZI UTAONA YAFUATAYO.
°Vifaranga wakiona baridi , hujikusanya karibu zaidi na chanzo cha joto. au wao wenyewe hujikusanya pamoja kwenye pembe ya kitalu au nyumba na hulia kwa sauti. Ukiona hivi ongeza kiwango cha joto adi waonekane kutawanyika kote kitaluni.
°Katika mduara/ kitalu cha kulea vifaranga mfugaji anatakiwa kufuatilia na kutambua kama hali ya joto iliyopo inawafaa vifaranga au la. Ufuatiliaji wa karibu utamsaidia kuchukua hatua mapema endapo marekebisho yatahitajika. Hii utafahamu kwa kuangalia tabia ya vifaranga wanapokuwa ndani ya kitalu .
KAMA JOTO LINATOSHELEZA UTAONA YAFUATAYO
• Vifaranga vitalia kwa furaha,
• Vitakimbia kimbia,
• Vitakunywa maji,
• Vitachaguachagua takataka na
• Kuonyesha shughuli nyingi, zote hizi ni dalili nzuri kuwa joto linatosha.
KAMA JOTO LIKIZIDI UTAONA YAFUATAYO.
> Vifaranga wakikaa mbali na vifaa vya joto ni dalili kuwa joto limezidi.
> joto likiwa kali vifaranga hukimbia kutoka kwenye mwamvuli (kama umewekwa).
>Husinzia na huzubaa. Katika hali hii itabidi upunguze joto kwa
kupandisha taa juu na kama bado joto ni kali punguza vifaa vya joto na kuwapa vifaranga maji mengi ya kunywa.
KAMA KUTAKUWA NA UPEPO UNAOPULIZA KUTOKA UPANDE MMOJA UTAONA YAFUATAYO.
>Vifaranga watajikusanya upande mmoja wa kitalu mbali na upepo unakotokea. Kutegemeana na jinsi utakavyowaona vifaranga
wanafanya, kama wataashiria tatizo, fanya marekebisho mapema kabla hayajatokea madhara kwa vifaranga.
>Katika majuma 5 ya kwanza vifaranga huhitaji joto usiku na mchana na katika majuma 3 yanayofuata joto hujitajiwa wakati wa usiku tu. Hata hivyo ikumbukwe kuwa joto katika nyumba ya vifaranga hubadilika kufuata maeneo tofauti na pia kutegemeana na majira tofauti ya mwaka. Hivyo kama hali ya baridi ikizidi,
muda wa kuwasha taa urefushwe, wakati wa joto kali taa zinaweza kuzimishwa hata kama ni juma la kwanza au la pili.
>Jambo la msingi ni mfugaji kuwa macho na kuwapa vifaranga joto la kutosha mara tu hali ya hewa ikibadilika kuwa ya baridi ghafla.
>Hali ya hewa ikiwa nzuri madirisha yafunguliwe katika juma la kwanza au la pili kwa ajili ya kutunza matandazo sakafuni yasiwe na unyevu.
VIFARANGA HUOTA MANYOYA manyoya mapya wakiwa na umri wa majuma 5 – 6 lakini huotesha manyoya ya kutosha katika juma la 8. Wakiisha ota manyoya ya kutosha vifaranga wanaweza kuvumilia zaidi hali ya baridi. Ufuatiliaji wa karibu ni muhimu kwa kipindi chote cha majuma matano (5) ili kuepusha vifo visivyokuwa vya lazima.
WAONDOE VIFARANGA kwenye kitalu cha kuwalea mara tu wakiwa na manyoya ya kutosha, yaani katika juma la 4 -5 kutegemeana na hali yao ya manyoya na hali ya hewa iliyopo.
ULISHAJI WA VIFARANGA
>Chakula na Maji; Ili vifaranga wawe na maendeleo mazuri ya ukuaji, wanatakiwa wapewe chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ambavyo ni Protini, Madini, Wanga na Vitamin pamoja na maji safi wakati wote.
>Pia chakula kunaweza kuchanganywa na mchanga kidogo ambao husaidia usagishaji wa chakula kilicholiwa.
> Hakikisha vyombo vya maji vinakuwa safi wakati wote.
> Chakula na maji yabadilishwe kila baada ya masaa 24.
> Hakikisha vifaranga wanapewa chakula wanachoweza kumaliza katika masaa 24 ili kuzuia uharibifu.
>Siku 7 – 10 baada ya kupokea vifaranga vyombo vya mwanzo vya maji na chakula vibadilishwe wawekewe vyombo vya kawaida.
>Vifaranga wapewe maji safi , vyombo vya maji visafi shwe na kujazwa maji mara mbili kila siku. Kila asubuhi sehemu zilizo na vyombo vya maji zikaguliwe na takataka zenye unyevu
ziondolewe.
>Vyombo vya chakula vijazwe nusu hasa vifaranga wakiwa na umri wa siku 10 – 14. Pia vifaranga wakiwa na umri huo huo wapewe majani mabichi yaliyo bora na yenye thamani.
>Majani yafungwe mafungu na kuning’inizwa kwa kamba.
VYOMBO VYA VYAKULA NA MAJI.
Waweza nunua, hii inategemea na hali ya mfugaji.nVyombo vya chakula na maji vinaweza kuwa ni makopo, sufuria, karai n.k. Pia vinaweza kuundwa kwa kukata madebe, galoni za plastiki, vibuyu n.k. Aidha vyombo hivyo vinaweza kutengenezwa kwa kutumia mbao, mianzi, Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa vyombo hivyo haviruhusu kuku kuchafua chakula au maji. Mfano kuna vyombo vya chakula na maji ambavyo mfugaji anaweza kujitengenezea.
•Vifaranga wakiwa bado wadogo anaweza kutumia sahani za chakula kuweka kokoto safi na kuzitumia kunyweshea vifaranga maji.
MFANO WA KILO 100 ZA CHAKULA CHA VIFARANGA.
Aina ya vyakula Kiasi ( Kilo)
*Nafaka kama mahindi au mtama kg 40
*Pumba za mtama, mahindi, uwele,kg 27
*Mashudu ya, alizeti, ufuta, karanga, au soya kg 20
*Unga wa mifupa, chokaa kg 2.25
*Dagaa au mabaki ya samaki kg 10
*Chumvi ya jikoni kg 0.5
*Virutubisho (Premix) kg 0.25
Jumla 100
NB; Vifaranga wanatakiwa kupata chanjo zote za awali na mwendelezo wa chanjo hizo kulingana na taratibu za chanjo zilivyo.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI