Viazi mviringo ni moja kati ya zao
ambalo kamwe uhitaji wake hauwezi kupungua bali unazidi kuongezeka kadiri siku
zinavyokwenda na kwa umaarufu wake kutumika kupika mapishi mbalimbali ya
majumbani na mahotelini.biashara ya viazi aka chips inalipa sana sio kwa
mkulima tuu bali hata mpishi au muuzaji wa vyakula. sokoni kariakoo kilo moja
ya viazi ni kati ya shilingi 1300-1500 (Kariakoo market cooperation)
na kwa mikoani ni kati ya shilingi 800-1000. Kwa hiyo kwa mkulima mdogo wa
hekari moja anaweza kupata faida ya kuazia milioni tatu na kuendelea kwa msimu
mmoja (3,000,000/=)
I. UTANGULIZI:
Viazi mviringo au kwa jina jingine
viazi ulaya ni jina ambalo hutumika kutofautisha zao hili na zao la viazi
vitamu. Zao hili ni muhimu kati ya mazao ya mizizi katika maeneo ya miinuko ya
Afrika mashariki.
Katika maeneo ya miinuko zaidi, zao
hili huwa na mavuno makubwa zaidi kwa zao la mahindi na hukua kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
Viazi mviringo hutumika sana kama
zao kuu la chakula hapa nchini na pia husafirishwa katika maeneo ya mbali kama
vila Kampala, Mombasa na Dar,es salaam.
Hapa Tanzania viazi mviringo
kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya kaskazini kama vile Moshi, Arusha,
Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko kama vile Njombe mkoani Iringa na
wilaya za mkoa wa Mbeya.Pia maeneo ya Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa
ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha zao hili kwa wingi.
II. MMEA WA KIAZI ULIVYO
Kiazi ni mzizi wa mmea unaovimba
ukiwa chini ya ardhi na kuwa na vijicho vingi, ambavyo baada ya miezi 2 – 3
vijicho hivi huchipua na kuota shina, kijicho kimoja huweza kutoa zaidi ya
shina 1 ambapo hutoa vitawi vingine.
Pingili zilizopo kwenye shina hutoa
mizizi inayomea chni ya ardhi na miisho yake huvimba na kuwa kiazi. Viazi
nyenye ngozi nyeupe huwa na maua meupe na ileyenye rangi hutoa maua ya rangi
aidha pinki, bluuau zambarau.Katika mzunguko wa ukuaji kiazi huendelea kukua
hata baada ya maua kutoka; ili mradi kuwe na na unyevunyevu wa kutosha kwenye
udongo na yasiwepo magonjwa.
II. HALI YA HEWA
Mvua:-
Viazi huhitaji mvua za kiasi cha
sentimita 25 kwa wiki ambazo hutakiwa kuendela kwa muda wa miezi 3 .5 hii
huweza kukuza viazi na kupata mavuno mazuri.
Joto:-
Viazi hukua vizuri zaidi kwenye
baridi kwa mwinuko wa mita 1,800 kulikoni kwenye joto. Maeneo machache ya
mwinuko wa mita 1,500 huweza kukuza viazi, japo pia hukua kwenye mwinuko wa
mita 2,900.
Udongo:-
Viazi hutoa mavuno mazuri kwenye
udongo usiokuwa mzito na unaopitisha maji kwa urahisi. Udongo wenye viini lishe
vya kutosha au kuongeza samadi na mbolea za viwandani.
IV. AINA ZA VIAZI
Aina zote za viazi zimeingizwa
Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.
Dutch Robijn - kutoka Holland
- ndani ni njano
- inavumilia kidogo ugonjwa wa
ukungu
- hushambuliwa sana na Mnyauko
Bakteria
- hupendwa na walaji wengi
ii. Roslin - kutoka Scotlland
- ngozi yake ni nyeupe
- ndani ni nyeupe
- huvumulia ugonjwa wa ukungu
iii. Kerr’s Pink -
ngozi yake ni nyeupe au nyekundu
- ndani ni nyeupe
- hushambuliwa sana na ukungu na
Mnyauko Bakteria
iv. Atzimba - kutoka Mexico
- huvumilia ugonjwa wa ukungu
V. MBEGU ZAKUZALISHA VIAZI
Viazi vyenye umbile dogo hutumika
kama mbegu, hutakiwa kuwa na upana wa sentimita 3 – 6. Kiasi cha robo tatu za
tani huhitajika kuotesha ekari 1 sawa na tani 1.85 kwa hekta 1.
Mbegu hazitakiwi kuhifadhiwa kwenye
giza nene kwani zitaanza kutoa vichipukizi virefu vyeupe.
VI. KUANDAA SHAMBA
Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta
vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hiihusaidia
kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi.
Inashauriwa pia kama matuta
hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini
kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo
mavuno huongezeka.
VII. KUOTESHA VIAZI
Viazi hutakiwa kuoteshwa mara karibu
kabisa na mvua zinapotaka kuanza kuchelewa kuotesha kutapunguza kipindi cha
ukuaji wa ile mizizi ili iwe viazi na hivyo kukabiliwa na kipindi cha ukavu.
Uoteshaji hufanyika kwa mikono na
mbegu ziwekwe chini udongo kwa kina cha sentimita 10. Kama mbegu zitaoteshwa
bila matuta basi zioteshwe kwa kina cha sentimita 15 na kufunikwa na udongo
mchache na wakati wa palizi udongo utaongezwa ili kuongeza utoaji wa viazi kwa
wingi. Nafasi ya kuotesha ni sentimita 75 toka mstari hadi mstari na sentimita
23 – 30kwa mche hadi mche.
VIII. MBOLEA
Viazi hustawi vizuri zidi kwenye
udongo ulioongezwa samadi na ni muhimu chimbiwe katika kina kirefu. Mbolea za
viwandani zinazotakiwa ni zile zenye Nitrogeni kwa kiasi cha kilo 22 – 45 kwa
ekari; zenye Chokaa P2O5 kwakilo 45 – 65 kwa ekari.
Ni vyema kuongeza mbolea na samadi
wakati kuna mategemeo mazuri ya mavuno kwa kuzingatia kuwa mbegu zilizooteshwa
hazina magonjwa ya aina yoyote.
IX. PALIZI
Zao la viazi likioteshwa kwa nafasi
zilizoshauriwa basi huweza kufunika ardhi yote na hivyo kugandamiza magugu, hii
husaidia kwa kipindi cha wiki 6 za mwanzo. Katika mpando wa matuta, basi huwa
ni kuondoa magugu na kujaza udongo kwenye mashina.
X. KUVUNA
Uvunaji wa viazi hufanyika kwa
kutumia jembe la mkono, viazi vikishang’olewa kutoka chini ya udongo visiachwe
kwa muda mrefu kwani vitabadilika rangi na kuwa kijani.
Ili kuifanya ngozi yaviazi kuwa
ngumu na isiharibike kirahisi basi mashina yote yanyofolewe wiki 2 – 3 kabla ya
kuvuta viazi juu ya udongo. Baada ya viazi kuvunwa haviwezi kuhifadhiwa kwa
muda mrefu kwani huanza kuchipua. Viazi huweza kuhifadhiwa kwenye ardhi, lakini
si zaidi ya wiki 6 kwani vitakabiliwa na magonjwa na kushambuliwa na minyoo
fundo.
XI. MAVUNO
Mavuno huwa mengi kama utunzaji wa
kitaalamu umezingatiwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti magonjwa, kutumia aina
zinazostahimili magonjwa. Kiasi cha tani 6 – 8 kwa ekari huvunwa,sawa na tani
15 – 20 kwa hekta.
KUHIFADHI:-
Uhifadhi wa zao hili ni mgumu, hivyo
inashauriwa kuwa sehemu iliyotengwa kwa biashara iuzwe mapema, sehemu ya
kutumia nyumbani ihifadhiwe katika banda au ghala safi lenye sakafu, lisilo na
unyevu, mwanga wala joto- liwe na hewa safi na ya kutosha. Vinginevyo
husababisha viazi kuota haraka. Viazi vilivyowekwa ghalani visilundikwe kwa
kina kirefu, visambazwe ili visipate joto.
XII. WADUDU
Vidukari:-
Ni wadudu wadogo wanoshambilia
majani na mashina kwa:
- kufyonza utomvu na kusababisha
kunyauka kwa mmea.
- Majani kujikunja kuelekea juu.
- Majani kuwa magumu
- Mimea kudumaa
- Pia hubeba vimelea aina ya virusi
ambao huathiri mimea.
- Pia hueneza ugonjwa wa virus.
Tiba:- Wakati wa utunzaji wa mbegu
za viazi ni muhimu kupiga dawa ya wadudu ili kuepuka kupuliza shambani kwani
dawa nyingi itapotea.
Nondo wa viazi:-
Wadudu huathiri viazi vilivyooteshwa
wakati ambao sio wa msimu wa viazi. Viwavi wanaoanguliwa huingia ndani ya viazi
na kusababisha kuoza. Pia huingia ndani ya viazi wakati vikiwa stoo.
Kuzuia:-
- Otesha viazi katika
kinachoshauriwa au zaidi ya sentimita 3 kwani kiwavi
aingiae ndani ya hawezi kuchimba
kina kirefu na inulia matuta wakati viazi vinakuwa, hii husaidia kuzuia nondo
kutaga mayai.
- Viazi vyote vilivyochimbwa ni
muhimu viwekwe kwenye mifuko na mapema kabla ya alasiri ili kuepuka nondo
kutaga mayai.
- Vikihifadhiwa stoo majani ya aina
ya LANTANA CAMARA yaweza kutumika.
-
Tiba:- Wakati viazi vikiwa stoo,
dawa ya unga ya Aldrin hutumika kwenye viazi vya mbegu.
Nyunyizia majani ya viazi wakati
mmea ukiwa na mwezi 1dawa aina ya Dipterex, Diazon, Thiodan, Permethrin,
ACtellic au Sumithion.
Kama ni viazi vya kula basi tumia
PYRETHRUM.
Minyoofundoo:-
Hushambulia viazi vilivyoachwa kwa
muda mrefu ardhini na kwenye ardhi iliyoathirika na mmomonyoko.
Kuzuia:-
- Usioteshe mbegu ambazo
zimeshambuliwa na wadudu.
- Andaa shamba mapema ili masalia
yote ya mazao yaweze kuoza ili
kutoruhusu makazi ya minyoo fundo.
Mbawakavu:-
Ni wadudu wadogo ambao hutafuna
majani na kuacha matundu matundu.
Kuzuia: Tumia dawa aina ya
Malathion, Thiodan
MUHIMU:-
Pamoja madhara ya wadudu pia hueneza magonjwa mbali mbali ya
mimea, hivyo kutunza shamba kuwa safi hasa kupalilia; kuchimba na kutupa mbali
maotea pamoja na masalia yote na kubadilisha viazi na vipando kama maharage,
mahindi, hupunguza madhara.
Comments
Post a Comment