UFUGAJI: JUA NJIA ZA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI.

UBORESHAJI WA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI.
1. UTOTOAJI WA VIFARANGA KWA KUTUMIA MAKOO BADALA YA VIATAMIO.
No automatic alt text available.
Kwa kuwa mfugaji mdogo hawezi kununua mashine ya kuangua mayai, maana ni ghali. Badala yake hutumia kuku wa kienyeji wenye asili ya kuatamia mayai ili wamuangulie vifaranga.
Pamoja na kuwa njia hii hutumiwa na wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji, lakini kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi kuhusu ufugaji wa kisasa wa kuku, matokeo yake huw si ya kuridhisha. Tatizo ni mfugaji kushindwa kuwapatia kuku hao mafunzo mazuri.
Iwapo kuku wanaoatamia watatunzwa vizuri, kwa mfano, kwa kuwapatia
A. Nyumba bora
B. Chakula cha ziada
C. Maji safi, salama na ya kutosha
D. Matibabu ya magonjwa.
Kuku hao watafanya kazi zote wao wenyewe.
2. VIOTA KWA AJILI YA KUATAMIA.
Image may contain: bird
Badala ya kuacha kuku wajichagulie viota wenyewe ni vizuri zaidi kuwawekea viota karibu na nyumba yako. Hii itafanya wao wenyewe kuwa na sehemu nzuri ya kutaga, hawatokuwa na tabia ya kuhamahama
Kiota kizuri kinaweza kutengenezwa kutokana na mbao za masanduku. Ukubwa wa kiota kimoja ni karibu sentimeta 60 mraba, yaani urefu ni sentimeta 60 na upana ni sentimeta 60.
Sehemu ya mbele itengenezwe kwa vipande vyembamba vya mbao. Pia unaweza kuweka pazia kwa mbele iliyoshikiliwa na vibao ili KUKU aweze kuingia na kutoka kwa urahisi na pia pazia ile itumike kama kinga ili kuku anapokuwa katika kiota aweze kutaga bila wasiwasi wowote ule.
Utengenezaji wa kiota ukikamilika, weka ndani nyasi au majani makavu. Malizia kazi kwa kunyunyizia kiota dawa ya kuua wadudu kabla hakijaanza kutumiwa na kuku kwa kuatamia.
3. SIFA ZA KOO ANAYEFAA KUATAMIA MAYAI.
Kabla ya kuanzisha kazi ya uatamiaji mayai, inakubidi kwanza pawepo koo aliye bora. Koo anayefaa kutumiwa ni yule aliye tayari kuatamia. Kioo anapotaka kuwa katika hali ya kutaga mayai huonyesha dalili zilizo dhahiri kabisa.
Iwapo Koo huyu ataachwa tu, atajitafutia sehemu ya kimya na kujitengenezea kiota. Atataga mayai humo na baadaye kuyaatamia.
Ukishampata kuku wa kuatamia mayai, kazi ya pili ni kuhakikisha kuwa kuku huyo anaendelea kuwa na hali ya kutaka kuatamia. Ili kuwa na uhakika wa jambo hili, muache atage mayai walau mawili au matatu kisha uyaondoe mayai yale na umuwekee mawe mawili au matatu yenye ukubwa wa mayai au viazi mviringo vilivyo laini na vyenye ukubwa wa mayai. Iwapo kuku huyo ataatamia mawe au viazi hivyo kwa muda wa masaa 24 bila kususa, basi elewa kuwa kuku huyo anaweza kuaminika, kwa hiyo mrudishie mayai halisi aendelee kuyaatamia.
NOTE. Zoezi hili lifanywe wakati wa giza au muda wowote ambapo kuku hayupo katika kiatamio ila jitahidi kuku asikuone na pia usishike mayai na mikono makavu unashauriwa kupakaa majivu katika mikono yako.
4. SIFA ZA MAYAI YA KUATAMIA.
Kabla kuku hujamuwekea mayai ya kuatamia, kwanza ni lazima mayai hayo yachunguzwe ili kuona kama yanafaa kuatamiwa. Mayai yenye dosari zifuatazo, hayafai kuatamiwa:
A. Mayai yenye makaka yanayokwaruzakwaruza
B. Mayai yenye nyufa.
C. Mayai yenye tumbo baya, marefu na membamba sana au yaliyo mviringo kama mpira, yenye miinuko mabonde kwenye kaka lake.
D. Mayai yaliyochafuka sana. Hata hivyo, mayai yenye uchafu kidogo yanaweza kusafisha kwa kitambaa safi ambacho kimelowekwa na kukamuliwa. Iwe ni mwiko kuosha mayai kwa kutumia maji.
Mayai yasiyokuwa na kasoro hizo yanafaa kuatamiwa.baada ya kuyachagua yahifadhi katika sehemu ambayo haina joto au baridi kali. Mayai yanapohifadhiwa ile sehemu panga ya yai ielekezwe juu. Ikumbukwe kuwa mayai kuanguliwa vizuri iwapo yameatamiwa mara tu baada ya kutagwa. Yasichukue muda zaidi ya siku 14.
Tutaendelea na utunzaji wa kuku anayeatamia, malezi ya vifaranga,kipindi cha kuku kulea vifaranga, ugonjwa mbaya wa vifaranga kudhibiti wake pamoja na usafi wa viota, vyombo vya kulia chakula na kunywea maji.



Comments