UGONJWA WA HOMA YA MATUMBO ( TYPHOID)
Huu ni ugonjwa hatari unaouwa vifaranga na kuku wakubwa pia. Huambukiza kuku na bata mzinga pia. Kama ilivyo kwa binadamu, ugonjwa huu husababishwa na bakteria na huambukiza kupitia yai au vyakula na maji vilivyochafuliwa na kinyesi au damu kutoka kwa ndege wenye maambukizi ya ugonjwa huu.
Ugonjwa huu huonekana kama magonjwa mawili. Kwanza hushika vifaranga au kuku ambao hawajakua sana na huchangiwa zaidi na uchafu wa kwenye mabanda. Pili huwakumba wale kuku wakubwa.

UENEZAJI...
A. Ugonjwa huu huweza kuenezwa kutoka kwa makoo yaliyo na ugonjwa huu kupitia mayai kwenda kwa kifaranga.
B. Ni vigumu kuudhibiti ugonjwa huu katika mabanda ambayo hayana sakafu ya saruji.
C. Tabia ya kuku kudonoana hueneza pia ugonjwa huu. Bakteria humuingia kifaranga au kuku kupitia vidonda vilivyosababisha na kudonoana.
D. Mayai yaliyoambukiza na ugonjwa huu yakiliwa na binadamu hudhuru afya zao pia.
DALILI ZA UGONJWA HUU....
A. KWA VIFARANGA.
1. Vifaranga wanaotokana na mayai yaliyoambukizwa huanza kufa mara baada ya kutoka katika kiangulio. Vifo huendelea sana na sana ndani ya siku saba za mwanzo.
2. Hutoa kilio cha kusikitisha mara kwa mara..
3. Hujaza kinyesi cheupe ( weupe wa chokaa ) kwenye mpango wa sehemu ya kutolea kinyesi (yaan mkunduni)
B. KUKU WAKUBWA.
1. Kupungua kwa ghafla kwa hamu ya kula na huwa na kuu mara kwa mara
2. Kuku huanza kusinzia.
3. Manyoya hulegea na hutibuka.
4. Vichwa huwa na rangi isipokuwa ya kawaida.
5. Kuku huhara Mavi yenye rangi ya njano au kijani kibichi au njano mbichi. Kuharisha huendelea kwa siku tatu hadi wiki kadhaa.
KINGA
A. Tenganisha kuku wagonjwa na wale wazima.
B. Chanja kuku wafikishapo umri wa wiki nane na kila mwaka.
C. Nunua vifaranga na kuku kutoka mashamba au vituo vya kutotolea ambavyo vinajulikana vizuri kutokuwa na ugonjwa huu.
D. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu wazikwe au kuchomwa kabisa.
E. Safisha vyombo vyote vya kulia na kunywea maji na sakafu na kuta za nyumba ya kuku kwa kutumia viuawadudu. Tabia hii ya usafi iwe ni ya muda wote.
F. Kuku wafugwe mbali na madimbwi ya maji.
G. Kabla ya kuagiza kuku kwenye nyumba walimokuwa kuku wagonjwa, hakikisha
1. Maandiko yote yameondolewa katika nyumba ya kuku na kuchomwa.
2. Sakafu na kuta zote za banda zisafishwe na kunyunyiziwa dawa na kuachwa wazi kwa wiki mbili au zaidi.
3. Vyombo vyote vya kulia na kunywea maji vioshwe pia na kuachwa vikauke.
TIBA.
Tibu kwa kutumia dawa typophrim au dawa aina ya eurolidone. Changanya pia dawa hiyo kwenye chakula na maji. Tumia pia terramycin

Comments
Post a Comment