KAMPUNI YA KUFUGA SUNGURA YA "THE RABBIT BLISS" SASA YAHAMIA JIJINI DAR
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa
Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben akizngumza na Ripota maalum
wa Globu ya Jamii alietembelea makao makuu mapya ya Kampuni hiyo,
yaliyopo eneo la Majohe, jijini Dar es salaam. Kampuni hiyo hivi sasa
ipo Dar es salaam ikitokea Jijini Arusha kulikokuwa na makazi yake ya
awali baada ya mmiliki wa sasa kununua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa
na mmiliki wa awali. Akizungumza katika eneo hilo, Bw. Ruben alisema
kuwa ufugaji wa Sungura ni mzuri sana na unafaida kubwa kwa mfugaji,
kwani unaweza kumuingia kipato kikubwa kama atazingitia taratibu zote za
ufugani, hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kufuga au kujifunza
ufugaji wa Sungura wasisite kufika kwenye ofisi zao zilizopo Majohe,
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji
wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben (kushoto)
akizungumza jambo na Mkurugenzi Mwena wa Kampuni hiyo ambaye pia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Republic ya nchini Kenya, Moses
Mutua wakati wakimuangalia mmoja wa Sungura anaefugwa kisasa katika
Shamba ya Sungura, lililopo Majohe, jijini Dar es salaam. Sehemu ya Mabanda ya kisasa kabisa ya kufugia Sungura. Baadhi ya Sungura wanaofugwa na Kampuni ya The Rabbit Blill. Moses Mutua a.k.a Mr. Rabbit akiwa kabeba mabox maalum ya Sungura wanaokuwa katika hali kuzaa.
Comments
Post a Comment