SOKO LA SUNGURA
UKWELI KUHUSU SOKO LA SUNGURA Habari ya majukumu ndugu wafugaji leo katika ukurasa huu nitazungumzia kuhusu soko la sungura hii ni kutokana na maswali ya watu wemgi wanaoniuliza kuhusu soko hasa mahali lilipo. Pia ni kutokana na utafiti niliofanya na kugundua kuwa wafugaji wengi wa sungura changamoto yao kubwa ni upatikanaji wa soko la uhakika la kuuza sungura wao Kwanza kabisa kabla ya yote napenda mfahamu kuwa soko la sungura ni kubwa kuliko hata idadi ya sungura iliyopo mtaani tatizo kubwa ni jinsi ya kulifikia soko hilo Katika ufugaji wa sungura soko limegawanyika katika aina tatu tofauti 1.soko la sungura wa mbegu 2.Soko la mkojo na kinyesi cha sungura 3.Soko la nyama ya sungura 1 SOKO LA SUNGURA WA MBEGU\ Hii ni aina mojawapo ya soko la sungura kwa sasa. Mfugaji wa sungura anaweza kuanzisha ufugaji wa wanyama hawa kwa minajiri ya kuzalisha mbegu bora ya sungura na kuuza kwa wafugaji wapya wanaoanza. Hii ni biashara inayolipa sana kwani mara nyingi su...