JIFUNZE KUJUA UPUPU ULIVYO

Huu ndio upupu, ni mmea unaoota porini maeneo ya mikoa ya kusini hasa kipindi cha kiangazi ni mmea unaotambaa na kutoa mbegu kama maharage iliyozungukwa na vitu mithili ya manyoya hii kitu ikikupata mwilini "inawasha" vibaya mno kiasi kwamba hakuna maelezo, unaweza hata kupoteza maisha kama ukikupata kwa wingi, pia mbegu zake ni chakula na pia ni Natural viagra shughuli yake ni zaidi ya kidawa vumbi cha Congo.

Upupu tulikua tunatumia kama silaha kwa walimu unavizia unaenda kumwaga kwenye meza yake na kiti, basi akijichanga na kuketi tu balaa lake hatokuja kusahau anaweza akavua mpk nguo hadharani kwa kuwashwa.

NB: Dawa ya kutuliza muwasho wa upupu ni ndogo sana kujipaka majivu ya moto ama mchanga uliopigwa na jua kali na kupata moto.1483455441199.png

Comments