Posts

Showing posts from May, 2017

CHANGAMOTO KUU YA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI

CHANGAMOTO KUU YA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI NI HII. Ufugaji wa kuku ni njia rahisi ya kujipatia kipato na lishe bora kwa kaya nyingi za vijijini na kwa wafugaji kibiashara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba: • Ufugaji hauhitaji mtaji mkubwa kuuanzisha. • Ni rahisi kuusimamia. • Faida inapatikana mapema. • Mali ghafi nyingi zinazohitajika zinapatikana kwa urahisi katika mazingira ya vijijini. • Kwa kipindi cha hivi karibuni, uzoefu unaonyesha kuwa soko la kuku wa kienyeji linakua na linaelekea kwenye kutokutosheleza wateja. Pamoja na kuwepo kwa fursa hii nzuri ya kujikwamua kiuchumi, bado haijatumika kikamilifu. Changamoto kubwa iliyopo ni namna ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya kuku. Wafugaji wa kuku wanapokuwa wameanza kuona matokeo mazuri ya shughuli hii wengi urudishwa nyuma na kuvunjwa moyo kuendelea kutokana na hasara zinazotokana na magonjwa. Tatizo hili limeendelea kwa sababu ya: • Kushindwa kuyatambua vizuri magongwa. • Kutofahamu njia za kuyadhibiti kwa cha...

tiba ya mpapai kwa kuku

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU Zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika mada hii taelezea baadhi ya dawa hizo. Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai Kuandaa Kata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi. - Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike. Kutumia (kwa kinga) - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi. Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia - Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha kilo 1. - Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. - Waweza kuongezea maji kidogo na...

“HYDROPONIC FODDER”

Image
JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA CHA “HYDROPONIC FODDER” NA NAMNA INAVYOWEZA KUKUPA MAFANIKIO MAKUBWA KWENYE UFUGAJI "CHAKULA BORA NA CHENYE GHARAMA NDOGO KWA MIFUGO"   Hydroponics ni utaratibu wa kuotesha mimea kwa kutumia maji bila kuhusisha mchanga/udongo kabisa. Mimea inaoteshwa katika chombo maalum “tray” ambacho kipo safi na kina matundu kwa chini ili kusaidia maji yasituame wakati unamwagilia mimea yako. Tuangalie mfano wa uoteshaji mbegu za ngano kwa njia hii ili zitumike kama chakula cha mifugo kama kuku, ng’ombe, mbuzi kondoo, sungura.n.k. VIFAA: 1.Tray ya plastic au aluminium yenye matundu (umbo lolote tu). 2. Chupa ya kunyunyizia maji (sprayer). 3. Mbegu za ngano au shayiri(chagua ambazo hazijambunguliwa). 4. Chombo cha kulowekea mbegu (ndoo au beseni itafaa). 5. Chujio la plastiki au unaweza tumia kitambaa. JINSI YA KUANDAA: 1. Pima uzito wa mbegu zako kisha zisafishe kuondoa takataka zote. 2. Weka maji kwenye ndoo au beseni kisha weka mbegu za...

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU Zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika mada hii taelezea baadhi ya dawa hizo. Dawa ya kutibu Homa ya Matumbo "Fowl Typhoid" ni Kitunguu swaumu Kuandaa •Chukua robo kilo ya vitunguu swaumu •toa maganda. •Kisha twanga •changanya na maji kiasi cha lita moja •chuja na kuwapa maji yake kwa muda wa juma moja.
Image
MBEGU BORA ZA NYANYA 1. EDEN F1 :- hii ni mbegu chotara ambayo stahimilivu sana katika kipindi cha masika cha mvua nyingi.(tani 45 kwa ekari) 2. ASSILA F1 :- hii ni mbegu chotara ambayo ni stahimilivu sana kipindi cha kiangazi(ukame) mvua chache.(tani 25 kwa ekari) 3. ANNA F1 :- hii ni mbegu chotara ambayo ni maalum kwa kilimo cha ndani yaani GREENHOUSE.(tani 74 kwa ekari) Hizi ndio mbegu chotara zinazopendekezwa sana na wataalamu wa kilimo kwani zina mavuno mengi sana na zinastawi vizuri kwa maeneo mengi ya Tanzania.

TAJIRIKA NA KILIMO CHA MIHOGO, MKOMBOZI WA WAKULIMA WA TANZANIA

Image
UTANGULIZI Mihogo ni miongoni mwa mazao ya mizizi ambayo ni muhimu sana kwa chakula, hasa maeneo yenye mvua kidogo na sehemu zenye ukame. Mihogo hutumika kama zao la kinga ya njaa ambapo mizizi yake hutumika kama chakula na majani yake pia hutumika kama mboga. Kutokana na baadhi ya maeneo ya nchi yetu kuwa na ukame, wataalamu wa kilimo wanasisitiza na kushauri mazao ya kinga ya njaa yalimwe. Na Mihogo ni miongoni mwa mazao hayo. Kwa hiyo basi, uangalizi wa shamba toka kuandaa shamba mpaka mavuno unatakiwa kuzingatiwa. HALI YA HEWA ,UDONGO UFAAO NA UTAYARISHAJI WA SHAMBA. Ni zao linalostahimili ukame,hustawi vizuri katika maeneo yenye joto la wastani kama ya ukanda wa pwani na yale ya mwinuko usiozidi mita 1500. Ili shamba la Mihogo listawi vizuri ni vyema lilimwe kwenye ardhi ya yenye rutuba ya wastani, udongo tifutifu au kichanga na mvua ya wastani. Unyevunyevu ukizidi na mbolea kuwa nyingi husababisha mhogo kukua sana sehemu ya juu na kutoa majani mengi. Endap...

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa

Image
Viazi mviringo ni moja kati ya zao ambalo kamwe uhitaji wake hauwezi kupungua bali unazidi kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda na kwa umaarufu wake kutumika kupika mapishi mbalimbali ya majumbani na mahotelini.biashara ya viazi aka chips inalipa sana sio kwa mkulima tuu bali hata mpishi au muuzaji wa vyakula. sokoni kariakoo kilo moja ya viazi ni kati ya shilingi 1300-1500 ( Kariakoo market cooperation ) na kwa mikoani ni kati ya shilingi 800-1000. Kwa hiyo kwa mkulima mdogo wa hekari moja anaweza kupata faida ya kuazia milioni tatu na kuendelea kwa msimu mmoja (3,000,000/=) I. UTANGULIZI: Viazi mviringo au kwa jina jingine viazi ulaya ni jina ambalo hutumika kutofautisha zao hili na zao la viazi vitamu. Zao hili ni muhimu kati ya mazao ya mizizi katika maeneo ya miinuko ya Afrika mashariki. Katika maeneo ya miinuko zaidi, zao hili huwa na mavuno makubwa zaidi kwa zao la mahindi na hukua kwa kipindi cha mwaka mmoja. Viazi mviringo hutumika sana kama zao kuu l...

UFUGAJI:- zingatia haya unapofuga

Image
KAMA MFUGAJI KUKU YASIKUPITE HAYA 1)Zingatia kuimarisha kinga ya mwili ya mifugo yako dhidi ya magonjwa kwa kuimarisha upatikanaji wa chakula bora na ziada ya protein na vitamin mimea ya kiasili kama aloevera mlonge na lusina ni mizuri kuimarisha kings 2)Epuka kuwapa kuku chakula Chenye uvundo au maji maji Hakikisha wanapewa chakula kikavu na ukisafirisha chakula kipindi cha mvua kuwa mwangalifu 3)Epuka kuwapa mifugo yako chakula dhaifu kwani athari zitaanzia tokea wakiwa vifaranha hadi kufikia kuku wanaotaga 4)ikiwa utatumia jiko la mkaa kama chanzo cha mbadala wa joto hakikisha moto was mkaa ni mwekundu na ufunikwe majivu moto was mkaa usipokuwa mwekundu utaleta gesi kwa vifaranga 5)jifunze kwa kina na uzingatie chanjo kwa maana chanjo na usafi ni msaada kwa afya.

UFUGAJI":- DALILI NA ATHARI ZA UPUNGUFU WA VIRUTUBISHI KWENYE CHAKULA CHA KUKU

 DALILI NA ATHARI ZA UPUNGUFU WA VIRUTUBISHI KWENYE CHAKULA CHA KUKU   1.Kuku hudumaa kukua 2.kuku hupungua uzito 3.Kuku hulemaa viungo 4.Kuku watagaji hutaga mayai yenye maganda laini 5.Kuku hupunguza utagaji wa mayai au hutaga mayai machache 6.Kuku hujaa tumbo,kifua na ngozi 7.Manyoya ya kuku hujikunja au kunyonyoka 8.Kuku kutoota manyoya ya kutosha. 9.Kuku huvunjika mifupa kwa urahisi TIBA-ili kuwarekebisha wape virutubishi vilivyopungua katika chakula.Chakula cha kuku kinatakiwa kiwe na: 1-WANGA-Chanzo chake ni kama vile Mahindi,ngano,Mtama,Sukariguru,Mabaki ya Viwanda vya bia (machicha ya mtama,shairi au ngano),Unga wa muhogo n.k   2.PROTINI- Chanzo kutoka kwa mimea kama vile maharage ya soya,Alizeti (mashudu ya alizeti),Pamba (mashudu ya mbegu za pamba), Ufuta ( mashudu ya mbegu za ufuta) karanga (mashudu ya karanga  chanzo kutoka kwa wanyama kama vile Dagaa (fishmeal)(unga wa dagaa),Damu (Damu za ng'ombe/Blood meal) n.k 3.VI...