UFUGAJI":- DALILI NA ATHARI ZA UPUNGUFU WA VIRUTUBISHI KWENYE CHAKULA CHA KUKU



 DALILI NA ATHARI ZA UPUNGUFU WA VIRUTUBISHI KWENYE CHAKULA CHA KUKU

 
1.Kuku hudumaa kukua

2.kuku hupungua uzito

3.Kuku hulemaa viungo

4.Kuku watagaji hutaga mayai yenye maganda laini

5.Kuku hupunguza utagaji wa mayai au hutaga mayai machache

6.Kuku hujaa tumbo,kifua na ngozi

7.Manyoya ya kuku hujikunja au kunyonyoka

8.Kuku kutoota manyoya ya kutosha.

9.Kuku huvunjika mifupa kwa urahisi

TIBA-ili kuwarekebisha wape virutubishi vilivyopungua katika chakula.Chakula cha kuku kinatakiwa kiwe na:

1-WANGA-Chanzo chake ni kama vile Mahindi,ngano,Mtama,Sukariguru,Mabaki ya Viwanda vya bia (machicha ya mtama,shairi au ngano),Unga wa muhogo n.k

 
2.PROTINI- Chanzo kutoka kwa mimea kama vile maharage ya soya,Alizeti (mashudu ya alizeti),Pamba (mashudu ya mbegu za pamba), Ufuta ( mashudu ya mbegu za ufuta) karanga (mashudu ya karanga

 chanzo kutoka kwa wanyama kama vile Dagaa (fishmeal)(unga wa dagaa),Damu (Damu za ng'ombe/Blood meal) n.k

3.VITAMINI-chanzo mboga zenye rangi ya kijani,Vitamini vilivyotengenezwa viwandani.


4.MADINI-Chanzo nin unga wa mifupa,madini yaliyotengenezwa viwandani,Chokaa,Maganda ya mayai na konokono.

KINGA- Walishe kuku wako chakula chenye mchanganyiko wenye uwiano sahihi wa  wa wanga,protini ,vitamini na madini pamoja na maji safi na salama  ya kutosha.

KUMBUKA-Maji ya kutosha ambayo ni safi na salama nayo ni muhimu sana kwa kuku wako.

MUHIMU- kuku watagaji wanahitaji wapate virutubisho vyote muhimu na maji ya kutosha kwani 74% ya yai ni maji.Pia Kasham (CALCIUM) na protein ni muhimu sana kwa kuku na visipo patika kwa wakati na kutosha watapunguza au kutotaga kwa uhakika (watakuwa kuku wa nyama),Maji,Kashamu na maji ni muhimu sana kuku wako wanapofikisha miezi 7 hadi 8 kwani ni kipindi ambacho wanakuwa wamefikia hatua ya utagaji kamili.Pia  wapate vitamini,madini mengine ya ziada kwa ajili ya uzalishaji mzuri wa mayai.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa