tiba ya mpapai kwa kuku

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU
Zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika mada hii taelezea baadhi ya dawa hizo.
Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai
Kuandaa
Kata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu.
Kutumia (kwa tiba)
- Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi.
- Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.
Kutumia (kwa kinga)
- Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi.
Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia
- Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha kilo 1.
- Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2.
- Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone.
Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa