CHANGAMOTO KUU YA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI

CHANGAMOTO KUU YA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI NI HII.
Ufugaji wa kuku ni njia rahisi ya kujipatia kipato na lishe bora kwa kaya nyingi za vijijini na kwa wafugaji kibiashara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba:
• Ufugaji hauhitaji mtaji mkubwa kuuanzisha.
• Ni rahisi kuusimamia.
• Faida inapatikana mapema.
• Mali ghafi nyingi zinazohitajika zinapatikana kwa urahisi katika mazingira ya vijijini.
• Kwa kipindi cha hivi karibuni, uzoefu unaonyesha kuwa soko la kuku wa kienyeji linakua na linaelekea kwenye kutokutosheleza wateja.

Pamoja na kuwepo kwa fursa hii nzuri ya kujikwamua kiuchumi, bado haijatumika kikamilifu. Changamoto kubwa iliyopo ni namna ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya kuku. Wafugaji wa kuku wanapokuwa wameanza kuona matokeo mazuri ya shughuli hii wengi urudishwa nyuma na kuvunjwa moyo kuendelea kutokana na hasara zinazotokana na magonjwa.
Tatizo hili limeendelea kwa sababu ya:
• Kushindwa kuyatambua vizuri magongwa.
• Kutofahamu njia za kuyadhibiti kwa chanjo na kwa njia nyinginezo hata za asili.
• Kutofahamu tiba sahihi ya magonjwa hayo.
• Kutofahamu taratibu za ufugaji zinazoweza kupunguza matukio ya magonjwa.
Madhumuni ya makala hii ni kumpa mfugaji mwongozo aweze kutambua dalili za magonjwa mbali mbali ya kuku kwa kina na jinsi ya kuyakinga na kuyatibu. Hatimaye aweze kuwa msaada kwa wafugaji wengine. Mambo yafuatayo yataelezwa katika makala hii:
• Magonjwa ya kuku yanayotokana na virusi.
• Magonjwa ya kuku yanayotokana na bakteria.
• Magonjwa ya kuku yanayotokana na protozoa.
• Wadudu wasumbufu katika kuku.
• Chanjo muhimu kwa kuku.
• Kanuni muhimu za kudhibiti magonjwa

Comments