MENGINEYO: JINSI YA KUTENGENEZA MBOLEA YA MAJI
Mimea inaweza kukuonyesha inahitaji nini. Ni rahisi sana kugundua endapo mimea haipati virutubisho vya kutosha. Majani kubadili rangi ni ishara tosha kuwa mimea ina upungufu wa virutubisho. Ni lazima mkulima awe tayari kutatua tatizo hilo kwa haraka kabla hali haijawa mbaya. Upungufu wa madini ya nitrojen na fosiforasi ni jambo la kawaida kwa mimea. Virutubisho hivi vinahitajik kwa kiasi kikubwa sana kwenye mimea hasa katika hatua ya ukuaji. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba utatuzi unategemea hatua za kutunza udongo kwa kipindi chote cha mwaka. Lisha udongo ili ulishe mazao yako; tumia mboji, samadi, mbolea vunde, matandazo na utaratibu mzuri wa kupanda mazao kwa mzunguko. Kunyunyizia kunafaa zaidi Mkulima anaweza kusaidia hatua hii ya kulisha mimea inayokuwa kwa njia ya kunyunyizia mbolea ya maji. Kunyunyizia inasaidia kuipatia mimea virutubisho moja kwa moja kupitia kwenye majani na shina. Unaweza kuona matokeo mazuri ya kuweka...