ni namna gani unaweza kufuga mbuzi wa maziwa
KWA ufugaji
wetu wa asili, tumezowea tu kuwalisha mifugo chochote ambacho wanaweza
kukipata, hususan nyasi na majani ya miti. Huo ni ufugaji wa mazowea!
Naam.
Tunawapeleka ng’ombe au mbuzi mbugani au vichakani ambako wanapata lishe bora
ya asili, jambo ambalo ni jema kwa sababu kadiri mifugo inapopata chakula cha
aina tofauti ndivyo inavyotengeneza mseto mzuri wa nyama au maziwa.http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Hata hivyo,
linapokuja suala la ufugaji wakibiashara ambao una malengo ya kutengeneza kipato badala ya kufuga kwa
ufahari kama tulivyozowea, ni lazima kujua namna nzuri ya kuihudumia mifugo
yetu.
Ni lazima
tutambue kwamba tunafuga kwa kufuata program inayoendana uzalishaji na ili
kuyafikia malengo yetu ni lazima tuzingatie umakini katika kutunza mifugo hiyo.
Ndani ya MaendeleoVijijini ninazungumzia mambo
mengi ya namna ya kuwahudumia mbuzi – iwe wa maziwa au nyama –
maelezo ambazo yatawafaa wafugaji wote wa mbuzi bila kujali kama wanafuga kwa
ajili ya maziwa au nyama.
Humu ninaelezea
kuhusu namna ya
wako wanapokuwa kwenye joto, namna ya kuwatunza
madume, namna ya kuwatunza mbuzi kabla hawajafikia umri wa kuzaa, ukamuaji wa maziwa, , na mambo
mengine mengi.http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Kila
kipengele kitafafanuliwa vyema ili kwa kila mfugaji wa mbuzi wa jamii mojawapo
aweze kujua nini cha kufanya katika kuboresha ufugaji wake.
Ulishaji wa mbuzi
Lishe ni
jambo muhimu kwa kiumbe yeyote – iwe mnyama, mdudu au mmea katika kujenga mwili
na kuzaa matunda. Hivyo, ni vyema kabisa kutambua kwamba, chakula unachomlisha
mbuzi wako ndicho kitakachotengeneza maziwa
au nyama.
Kwa maana
hiyo, ni vizuri kutambua kwamba kumpa mbuzi chakula mahali pasipo safi si jambo
jema kwa sababu mbuzi hula kila aina ya chakula kwa hiyo usiwaruhusu kula
chakula kilicho na mchanga. Kuwalisha chakula kilichochanganyika na mchanga
kunawafanya wawe katika uwezekano mkubwa wa kupata minyoo wanaopatikana kwenye
mchanga.
Unaweza
kuwafungulia mbuzi wako ili wale nyasi shambani na majani ya miti vichakani, hilo
ni jambo jema, hasa unapokuwa na eneo kubwa la shamba ama uko kijijini ambako
maeneo ya malisho ni mengi.
Lakini mbuzi
wa maziwa mara nyingi hufugiwa kwenye mabanda kwa mfumo wa ‘zero grazing’, kwa
hiyo ni lazima kuwatengezea mahali pa kulia chakula na kunywea maji ambapo
panahitajika kuwa juu na mbali na nyumba yao ya kulala ili wasikanyage au
kuchafua chakula.
Kwa kawaida,
mbuzi mwenye uzani wa wastani huhitaji takriban nusu tani au kilo 500 za
chakula cha hali ya juu ama nyasi zilizokaushwa kwa mwaka huku kiwango cha kila
siku kikiwa asilimia 5-7 ya uzito wake.
Kupanga
chakula cha mbuzi wa maziwa ni tofauti na kupanga chakula cha paka, mbwa ama
binadamu. Kama walivyo ng’ombe, mbuzi pia ni wanyama wanaocheua (ruminants).
Matumbo yao yamegawanyika katika sehemu nne na wanakula nyakula vyenye asili ya
mimea ambavyo vina wanga wa kutosha pamoja na maji.
Mbuzi pia
wanategemea vijidudu ndani ya matumbo yao ili kumeng’enya vyakula. Hii ni
sayansi ambayo kwa yeyote aliyepita darasani anaweza kuikumbuka. Wakati chakula
kigumu kinapoingia kwenye sehemu ya utumbo mpana (rumen) na reticulum, wadudu
jamii ya protozoa na bakteria hukimeng’enya na kukiweka katika mfumo mwingine
ambao utamwezesha mbuzi kukitumia kwa ajili ya shibe, kukuza mifupa, misuli,
manyoya pamoja na kutoa maziwa. Kwa namna nyingine, unawalisha wadudu, na
wadudu wanamlisha mbuzi.
Hii maana
yake ni kwamba mbuzi anaweza kutumia kiasi kikubwa cha chakula, hususan nyasi.
Mbuzi mzuri
katika utoaji wa maziwa pia anahitaji uwezo mkubwa wa kula nyasi za kutosha.
Nyasi aina ya alfalfa mara nyingi zinapendekezwa kwa ajili ya ulishaji wa mbuzi
wa maziwa, kwa sababu zina wingi wa protini na madini ya kalsiumu. Hata hivyo,
nyasi hizo hazipatikani kila mahali, hivyo unaweza kutumia nyasi nyingine
mbadala ambazo ni laini.
Majani kama
vile napier, majani ya mahindi au mtama, mboga zisizotumiwa na majani ya viazi
yanapaswa kukakatwa ili kupunguza uharibifu. Pia nyasi kavu za ngano au mpunga
ni chakula kizuri kwao. http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Wakati wa
masika unaweza kukata nyasi nyingi na kuzianika halafu uzihifadhi vizuri kwenye
banda maalum ili ziwafae kwa ajili ya kiangazi ambapo nyasi huwa shida
kupatikana.
Kama chakula
ulichowalisha bandani kimebakia, hakikisha unakiondoa na kumbuka tu kwamba,
kama mbuzi wako wanabakisha chakula kingi hii ni ishara kwamba chakula hicho ni
duni, ama unawapa chakula kingi kupita kiasi, au mbuzi wako hawana hamu ya kula
chakula kwa sababu wana tatizo kama vile kutojihisi vyema au minyoo.
Unaweza
kuwapa mbuzi nafaka kama njia ya kubadilisha chakula tofauti na kile cha
kawaida, lakini tahadhali, zoezi la kuwabadilishia chakula cha nyongeza lazima
lifanyike polepole na siyo mara moja ili kuwaruhusu mbuzi kuzowea chakula kipya
bila kuwadhuru. Kamwe usiwape mbuzi nafaka tupu kwa sababu zinaweza kusababisha
matatizo ya tumbo.
Unaweza pia
kuwalisha mbuzi wa maziwa vyakula vya maziwa vinavyolishwa na ng’ombe katika
kiwango cha nusu kilo kwa mbuzi asiyekamwa, kilo moja kwa mbuzi wa kukama lita
moja ya maziwa na nusu kilo kwa kila lita zaidi ya maziwa.
Hakikisha
unawalisha mbuzi madini muhimu kulingana na kiwango cha maziwa wanachotoa.
Wafugaji
wengi wa mbuzi hupendelea kutengeneza chakula cha nyongeza wao wenyewe ili
kuokoa fedha, kukifanya chakula hicho kiwe cha asili, au kwa sababu wana nafaka
nyumbani, jambo ambalo ni zuri.
Unaweza
kuchanganya nafaka, lakini kamwe haiwezi kuwa gharama rahisi, na itakuwa kazi
kubwa. Nafaka hizo zinatakiwa kupondwa au kusagwa katika mchanganyiko huo.
Unatakiwa kuongeza kiasi cha madini na protini ili kuweka uwiano mzuri.
Utakapopiga gharama ya mchanganyiko huo na muda uliotumia na vifaa itachukua
muda kuviandaa, utaona bora ukanunue.
Kama unalima
bustani, mabaki ya mboga mboga kama mchicha, karoti, kabichi, spinachi, sukuma
wiki na nyinginezo ni muhimu kwa malisho ya mbuzi wako, lakini hakikisha
umeyasafisha ili yasiwe na mchanga ambao unaweza kuwa na wadudu wengine
watakaoleta madhara kwa mbuzi wako.
Jambo
jingine muhimu ni kwamba, unapaswa kuwapa maji safi ya kunywa kwa wingi kama
lita 5 kwa kila mbuzi wa maziwa kwa siku.
Utunzaji
wa kumbukumbu
Kuweka
kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua kosaafu,
gharama za utunzaji na faida na humsadia mfugaji kufanya uamuzi katika kuendeleza
ufugaji wake.
Ikiwezekana
mtumie mtaalam wa mifugo ambaye atatumia kumbukumbu hizi ili kukusaidia kuboresha
ufugaji wako .http://kijanaendelevugroup.blogspot.com/
Ni muhimu sana
kuweka kumbukumbu hizi:
• Kumbukumbu
za idadi na ukuaji wa wanyama waliopo, jinsi zao, uzito wa kwa kila mwezi ili
kufuatilia ukuaji wao, tarehe ya kuachishwa kunyonya na idadi ya waliouzwa.
• Kumbukumbu
za uzazi zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi yake, aina
(breed), namba ya dume/jike, na uzito wa kuzaliwa.
• Kumbukumbu
za upandishaji zinazoonyesha namba ya mbuzi anayepandwa, tarehe ya joto na ya
kupandwa, namba ya dume lililotumika kupanda, tarehe ya joto la pili kama
atarudia na tarehe ya kuzaa.
• Kumbukumbu
za chanjo na matibabu zinazoonyesha namba ya mbuzi, tarehe ya matibabu, aina ya
chanjo au ugonjwa, dawa iliyotumika, idadi ya waliokufa na waliopona na jina la
mtaalam aliyetibu.
• Kumbukumbu
za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi, tarehe ya kuzaa, kiasi cha maziwa kwa
siku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chote cha kukamuliwa, tarehe ya kuacha
kukamua na idadi ya siku alizokamuliwa.
• Kumbukumbu
za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi, vitu vilivyouzwa au
kununuliwa kwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa nacho kila wakati, kiasi cha
fedha unachodai na kudaiwa.
Comments
Post a Comment