KILIMO: kilimo cha minazi

UPANDAJI Uko wa ina mbili kuna wa vibox na wga pembetatu lakini kwa aina zote mbili umbali wa kupanda ni mita 7 .2 kutoka shimo hadi shimo la mnazi, kiasi cha mashimo 182 kwa hecta huingia na kama utatumia mtindo wa pembetatu basi mashimo 15 zaidi yataingia kwa hecta. Ukubwa wa shimo uwe futi tatu kwa kina, upana na urefu hi kwa maeneo yenye udongo mzuri na wakaida lakini maeneo yenye changarawe, mawe mawe na miamba ukubwa uongezeke hadi futi4 kwa mapana , urefu na kina, Shimo lijazwe majani kiasi cha kilo 15 – 20 unaweza kukisia kama theluthi moja ya shimo au futi moja baada ya kushindilia majani, weka juu yake kama, weka udongo wa juu (top soil) kiasi cha futi moja tena ongezea kiasi cha kilo 10 – 20 cha mbolea ya samadi. Hakikisha haijai na kufunika shimo lote, pia kama utapata ule udongo mwekundu ambao wengi hupenda kuutumia kwenye bustani zao, pia weka humu kiasi kama utaukosa basi acha vivo hivyo, anza kumwagilia maji wiki moja kabla ya kupanda mbegu yako, kama shimo litatitia ongezea udongo wenye rutuba ya kutosha, kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanyia maji, ila kama ni sehemu ambazo hufurika kipindi cha mvua jaza udongo hadi kuweka tuta ili maji yasituame.

 MAGONJWA YA MINAZI - KUOZA VIKONYO Huanza kwa majani machanga mawili ya mwanzo kubadilika rangi na kuwa njano na baadae huwa na vidoti vyeusi hutokea kwenye ukingo, majani hunyauka na kukauka na kisha sehemu ya chini linapoanzia jani huoza na kutoa harufu mbaya ambapo baadae mnazi wote hufa. Ili kuzuia ugonjwa huu mara tu unapoona dalili za mwanzo tengeneza mchanganyiko ufuatao (gramu 100 za copper sulphate changanya na nusu lita ya maji) + (Gramu 100 za chokaa changanya na nusu lita ya maji) kila moja itengenezwe peke yake halafu kisha vichanganywe pamoja baadae kisha pulizia kwenye minazi iliyoanza kushambuliwa, kama mnazi umeshambuliwa sana ukatwe na kuchomwa moto kuzuia maambukizi zaidi. Pia pulizia mchanganyiko huu msimu wa baridi kuanzi mwezi wa 5 hadi wa 9 kwenye shamba lako kama kinga.

- KUOZA MAJANI Majani huwa meusi kwenye ukingo na kuti likiliwa zaidi kati kati, majani machanga yakichomoza huwa dhaifu na kisha huchanguka, mnazi haufi ila mazao huwa duni kama ni mnazi unaozaa ili kuzuia tumia dawa yoyote ya kuzuia fangasi za mimea kama Hexaconazol, Mancozeb au Dithane - M5, muhimu ukufika duka la pembejeo ulizia dawa ya kuua fangasi wa mimea utapata dawa na maelekezo ya kuchanganya usikariri haya majina ya dawa nilizotaja

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI

jifunze kujua viazi mvirongo na faida zake hapa