TENGENEZA PESA KWA KUTUMIA BLOGSPOT

TENGENEZA PESA KWA KUTUMIA BLOGSPOT
Kila mtanzania ana ndoto ya kuwa na maisha mazuri ila wengi wetu tuna shindwa kutoka kimaisha kwasababu tu hatuzijui fursa zetu ,kuna niia mbali mbali wewe kama kijana unaweza kujiajili na kujikimu kimaisha ,
Unaweza kuanzisha blog yako inayo weza kukutengenezea pesa kwa namna moja ama nyingine yote haya utajifunza hapa hapa katika Makala zetu za technologia hii mpyaa 
Unaweza kutengeneza pesa kwa kuanzisha blog yako kwa kuweka matangazo ya watu pia wewe kama ni mfanya biashara unaweza ukaitangaza biashara yako duniani kote kwa kupitia blog yako hivo basi Tuangalie namna ya kuanzaa blog yako.



Hapa ndio mahali husika katika kujifunza namna ya kuwa na blog yako na kuifanya iwe na mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wamefanikiwa kupitia blog zao.

Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako.
NJIA YA KWANZA
BLOGGER Kupitia uwanja huo au platform hiyo inayomilikiwa na Google unaweza kuanzisha blog yako mwenyewe ambayo itabebwa na jina ulipendalo wewe mfano:- http://jinalablog.blogspot.com, hapo ambapo nimekoleza kwa maandishi ya rangi nyekundu ndipo ambapo utaweka jina la blog yako. Utaratibu mzima utaupata wakati ukiwa unaisajiri blog yako Bofya hapa ili kutengeneza blog yako Create a new Blog 
NJIA YA PILI
WORDPRESS Hapa pia utaratibu ni kama hapo mwanzo ila hizi ni nyanja (Platforms) tofauti na zinatofautiana vikolombwezo (features)  vya uboreshaji wa blogs. Hapa ukianzisha blog yako itabebwa na uwanja au platform ya wordpress. Namna ya jina la blog yako itakuwa katika mfano huu:- http://jinalabloglog.wordpress.com. Ukitaka kuwa na blog kupitia wordpress tafadhali bofya hapa, Sign up For New Wordpress
Naamini hadi sasa umeisha elewa namna ya kuweza kuanzisha blog yako, wakati mwingine nitazungumzia jinsi ya kuweza kuwa na blog yako ikiwa na domain yako mwenyewe mf:- www.domainyako.com. Endelea kusoma Makala zetu ili upate kujua mengi Zaidi na uweze kujua namna mbali mbali ambavo watu wana wini kimaisha.
IFANYE BLOG YAKO KUWA NA MUONEKANO MZURI ZAIDI 
Kuna njia nyingi sana za kufanya blog yako iwe na muonekano wa kipekee na wenye mvuto kwa kila atakae ingia katika blog yako nitakufundisha chache na rahisi ili upate kuelewa upesi na kuifanyia kazi blog yako kuanzia sasa
HTML ni aina ya lugha inayo tumika kuaandaa web pages kwa kutumia hii hapa itaweza kutengeneza pages za blog yako katika muonekano utakao upenda wewe ,mara nyingi ili kuifanya page yako ipendeze kwa marembo ya aina mbali mbali itakulazimu pia utumie lugha ina itwa CSS.ni ligha inayo weza kuifanya page yako ikae katika muundo wowote upendao
Vile vile HTML inasimama badala ya   Hyper Text Markup Language. pia HTML ina maana zifuatazo
HTML is a markup language
A markup language is a set of markup tags
The tags describe document content HTML
Documents contain HTML tags and plain text
HTML documents are also called web pages
Katika HTML kuna kitu kinajulikana kwa jina la HTML Tags, je nini maana yake? Na hutumiwaje? Unapotumia html lazima utumie hiki kitu kwani bila ya Html tag huwezi kufanya lolote kwani ndio ufunguo wa lugha hii ya kutengenezea website. Html Tag inakuwa katika mfano kama huu ikiwa na maana kuwa ufungo wa neno unakuwa katikati ya mabano hayo yenye pembe (angle brackets). HTML Tags huwa mara nyingi huja kwa jozi, yaani kama kuna <html>basi lazima kuwe kuna</html> ikiwa na maana kwamba, ile ya kwanza ni ya kufungua na ya pili ni ya kufunga.
Ila kumbuka kuwa tag ya mwisho ambayo ndiyo ya kufunga huwa inafanana na ile ya kufungua isipokuwa tu hii ya kufunga lazima ianze na alama ya mkwaju "/” kabla ya kumalizia neno husika. Mfano <mfano>……………</mfano> na huwezi kukuta kitu kama hiki <mfano>……..</body>
HTML ELEMENT
Hii ni kila kilichopo baina ya tag mbili pamoja na tag zenyewe. Mfano <p>this is my first page</p> Hivyo basi, ukikutana na sentensi kama hiyo <p>this is my first page </p>basi ujue kuwa hiyo ni HTML Element.
Kumbuka kuwa kazi ya tag ni kuamrisha yale maneno yaliyo baina ya tag hizo mbili, kuwa kwa jinsi tag hizo zilivyohitaji. Nitakupa mfano lakini sio katika HTML ila nimetumia mbinu hii ili kukuelewesha. Tuchukulie mfano unataka maandishi yako yatembee, maandishi yenyewe labda ni haya "WEBSITE NZURI” na katika ujuzi wako ukaona kuwa tag inayofaa kuamrisha maandishi yatembee inaitwa <marquee>, hivyo basi katika kutengeneza kwako utaandika kama ifuatavyo: <marquee>WEBSITE NZURI</marquee>
Kuna program zinazotumika kuandikia tag zetu ili tuweze kutengeneza website kama vile,
Adobe Dreamweaver
Microsoft Expression
Web CoffeeCup HTML Editor
Lakini kwa kujifunza HTML nasisitiza sana kutumia Notepad na ni njia rahisi na bora sana katika kujifunzia kuliko kwenda mbali huko. Nadhani kila mtu anajua kuwa katika Windows kuna program ndogo inayoitwa notepad, program hii kazi yake sana utaona ni kuandikia maneno lakini ina umuhimu mkubwa sana kwani hutumika kutengeneza baadhi ya application ndogo ndogo za kompyuta. Hivyo kwa hii hii tutaitumia katika kutengeneza web page.
Kwa asiyejua kuifungua hii fuata maelekezo haya:
To start Notepad go to: Start All Programs, Accessories,kisha bofya   notepad itafunguka. Muonekano wake ni kama huu hapa chini: Sasa hapo ndipo tunapoandika HTML Tags ili kufanikisha utengenezaji wa web page. Ni kama ndoto kwani hakuna lolote litakalowekwa humo ndani isipokuwa ni maandishi tu, lakini itatokea kurasa nzuri kabisa ya tovuti. 

Notepad

Comments