NYANYA CHUNGU/NGOGWE(African eggplant)

NYANYA CHUNGU/NGOGWE(African eggplant)


Nyanya Chungu au Ngogwe ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni nyanya chungu ambazo ni za asili na zingine ni chotara sio chungu kama za asili. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi.
AINA ZA NYANYA CHUNGU
Gilo
Kumbai
Shum
ASILI YAKE
Nyanya chungu asili yake ni Afrika Magharibi, lakini kwa sasa ime sambaa Afrika ya kati na mashariki. Kutokana na ugunduzi wake Afrika magharibi, zao hili pia linalimwa huko Visiwa vya Karibi, Amerika kusini na baadhi ya maeneo ya kusini-magharibi mwa Asia. Nyanya chungu hulimwa kwa matumizi ya chakula, matumizi ya dawa, na matumizi ya mapambo.
HALI YA HEWA
Nyanya chungu za aina zote hustawi sana sehemu yenye jua na udongo wenye kupitisha maji vizuri na udongo wenye pH kati ya 5.5 na 6.8. Gilo ni aina ambayo hustawi sana kwenye joto la mchana ni kati ya 25°C na 35°C (77°F na 95°F). Kumba ni aina hustawi maeneo yenye joto sana la 45°C na unyevu kidogo, Shum ni aina inahitaji joto na unyevu ili kustawi. Hakuna aina ya Nyanya chungu inayovumilia kwenye baridi kali na hali ya majimaji.
UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.
UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu za nyanya chungu zinauzwa kutoka baadhi ya makampuni ila kuna njia ya kupata mbegu kutoka kwenye tunda. Chukua nyanya chungu iliyokomaa menya vizuri baada ya hapo kusanya mbegu zilizopo ndani ya tunda, baada ya hapo ziweke kwenye kipande cha karatasi ili zikauke katika sehemu isiyopitisha mionzi ya jua ya moja kwa moja. Mbegu zikisha kauka zinaweza kutunzwa kwa miaka mingi na kuendelea kutumika. mbegu lazima zioteshwe kwenye kitalu cha sentimita 15 (6 inch) au zaidi 20 cm (8 inch) ya safu. miche kutoka kitaluni inakuwa tayari kupandwa ikifika urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (6–8 inch) na iwe na majani 5–7. Mmea inatakiwa uwe na nguvu katika mashina na yenye nafasi ya sentimita 50 (20 inch) mbali ruhusu sentimita 75 (30 inch) ya safu.
UPANDAJI
Kutoka kwenye kitalu miche ifikiapo kimo cha sentimeta 15 hadi 20 au majani manne 5-7 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya “Ngogwe” hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.
MBOLEA
Zao hili unashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi au mboji kuongeza uzalishaji wa mazao. mmea wa nyanya chungu unahitaji sana madini.
UPALILIAJI & UNYEVU
Shamba la nyanya chungu linatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.
MAGONJWA &WADUDU
Nyanya chungu ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa
yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara yake si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.
UVUNAJI
Nyanya chungu huvunwa wakati zikiwa bado mbichi, hukomaa baada ya siku 100 mpaka 120 kutoka kupandwa, unashauriwa uvune kabla hazija badilika rangi . Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.
SOKO
soko la nyanya chungu linaonekana kuwa zuri maana wahitaji wake ni wengi, ila fanya utafiti ili kujiridhisha soko lake.

Comments