Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote MTI WA MBILIMBI (M-MBILIMBI) Huu ni mmea unaopatikana sana sehemu za pwani kama Zanzibar, Tanga, Dar es salaam, Kibaha n.k Ni mmea ambao hauwezi kuhimili ukame wala baridi kali na unastawi zaidi kwenye mvua za kutosha na udongo usiotuamisha maji kabisa. MATUMIZI Miaka mingi mbilimbi zimekuwa zikijulikana kwa matumizi ya achali ndio maana sehemu nyingine mbilimbi zilitungwa jina la PICKLE FRUIT. Utengenezaji wa achali uko wa kuchanganya vitu tofauti tofauti kama nyanya, vitunguu, pilipili, ndimu, malimao, chumvi, maembe n.k ambavyo vinankuwa katika vipande vidogo vidigo, unaweka kwenye chupa na kuanika juani kwa siku kadhaa (ingawa baadhi huupika mchanganyiko huu) Mbilimbi pia hutumika kutengenezea siki (vinegar) na mvinyo, hii mara nyingi hufanyika viwandani na sio majumbani kama ilivyo achali. Mbilimbi pia ni dawa kwa magonjwa kama chunusi, kifua na kukohoa na mengineyo mengi. Ili kutibu kukohoa unatakiwa utafune mbilimbi kama ...
Hizi ni baadhi ya njia ya kuikinga na Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles. Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki 4 hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani. Bawasiri husababishwa na nini Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu: Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu Sababu za kurithi – baad...
Viazi mviringo ni moja kati ya zao ambalo kamwe uhitaji wake hauwezi kupungua bali unazidi kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda na kwa umaarufu wake kutumika kupika mapishi mbalimbali ya majumbani na mahotelini.biashara ya viazi aka chips inalipa sana sio kwa mkulima tuu bali hata mpishi au muuzaji wa vyakula. sokoni kariakoo kilo moja ya viazi ni kati ya shilingi 1300-1500 ( Kariakoo market cooperation ) na kwa mikoani ni kati ya shilingi 800-1000. Kwa hiyo kwa mkulima mdogo wa hekari moja anaweza kupata faida ya kuazia milioni tatu na kuendelea kwa msimu mmoja (3,000,000/=) I. UTANGULIZI: Viazi mviringo au kwa jina jingine viazi ulaya ni jina ambalo hutumika kutofautisha zao hili na zao la viazi vitamu. Zao hili ni muhimu kati ya mazao ya mizizi katika maeneo ya miinuko ya Afrika mashariki. Katika maeneo ya miinuko zaidi, zao hili huwa na mavuno makubwa zaidi kwa zao la mahindi na hukua kwa kipindi cha mwaka mmoja. Viazi mviringo hutumika sana kama zao kuu l...
Comments
Post a Comment