JUA JINSI YA KUANDAA MICHE YA MIPAPAI
Uandaaji wa mbegu za mipapai imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watu,
leo nitaongelea uaandaaji wake mpaka kupanda na kupata miche yako
Mbegu tulizotumia leo ni LADY RED ambazo hufaahamika zaidi kama Malkia
FI toka nchini Taiwan na huzalishwa na kampuni inayojulikana kama
KNOWN-YOU kama zinavyoonekana hapo pichani
Fungua mbegu zako na uziweke kwenye chombo kisafi kisha jaza maji kiasi, ziloweke humo kwa siku 5 na kila siku badilisha maji
Siku ya 6 zitoe na uziweke kwenye kitambaa kisafi kukwepa mashambulizi
ya fangas, Funga vizuri na lowesha maji kitambaa chako na ukihifadhi
sehemu salama
Zoezi hili linatakiwa kufanyika ndani ya nyumba au banda ambalo litazikinga mbegu dhidi ya jua la moja kwa moja
Siku ya 7 ukifungua utaona baadhi ya mbegu zimeanza kupasuka na tayari
kwa kuanza kuota, panda mbegu zako moja moja kwenye viriba ambavyo
ulishaviaandaa kabla kwa kuvijaza udongo wenye rutuba, kama utaweka
mbolea hakikisha ilishaoza kabla, viriba viwekwe kwenye kivuli hasa
chini ya miti
Baada ya siku kadhaa mbegu zako zitaanza kuota kama inavyoonekana pichani
Udongo unatakiwa uwe wenye rutuba na usiotumisha maji
Hakikisha unamwagia maji kila siku angalau mara moja na hasa jioni wakati hali ya joto imepungua
Baada ya wiki 2 miche itakuwa imefikia kimo cha sentimeta tano, hapa
unaweza kuongeza mbole ya kukuzia kama ya kuku na pia kuondoa miche yako
kwenye kivuli na kuiweka juani kama njia ya kuandaa kukabiliana na hali
ya shamba (hardening off)
Comments
Post a Comment