LIMA KILIMO BORA CHA
MICHUNGWA
UTANGULIZI.
Mchungwa ni jamii
ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukandawa pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na
udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga,
Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki. Pia tunda la mchungwa
huliwa na binadamu ili kuongeza vitamini mwilini.
Hali ya hewa.
Michungwa huweza kukuzwamaeneo yenye
joto na hata yale yenye baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengineya citrus, ili
kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika joto la nyuz ijoto 15.5c
– 29c.
Kuandaa mbegu.
Mchungwa kwa kuanzia unakusanya
mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva
yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kasha unaweza kutolea ganda la nje ili
ziweze kuota vizuri.
Kuandaa kitalu.
Tengeneza kitalu chako vizuri kwa
kutumia jembe, kisha changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka
vema mwaga mbegu zako na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kasha
mwagia maji kila siku na baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kichipua, baada ya
miche kufikia kiasi cha sentimita 3 – 5, miche ihamishwe kwenye pakiti zenye udongo
(viriba) wenye mbolea ya kutosha na viwekwe kwenye kivuli kiasi.
Kuunga miche.
Miche ikifikia urefu wastani wa
sentimita 30 – 45 huungwa ili kupata michungwa. Kwa michungwa kuna aina mbili
kuu hapa Tanzania ambazo ni Jaffer na Valencia. Jaffer ni rahisi kuunga sababu
vikonyo vyake ni vikubwa na viko wazi kwenye miti, miti yake ni mikubwa na
inazaa sanalakini huathirika sana jua likiwa kali na matunda yake huanguka, pia
machungwa yake hukua kwa haraka sana ilasoko likiwa baya huishia shambani kwa kuanguka. Vlencia
ni miti ya wastani , vikonyo havipo wazi kwa hiyo huwapa kazi waungaji
(hawaipendi) ina uzao wa wastani na inakaribia ukame na matunda yake hayaivi
haraka.
Upandaji.
Baada ya uungaji kukubali unaweza
kuandaa shamba lako kwa kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kusubiri msimu wa
mvua, miche ipandwe mara tu baada ya mvua za kwanza kunyesha, umbali wa kupanda
ni mita 8 * 8 kwa Jaffer na mita 5 * 8 kwa Valencia.
Palizi na matumizi ya mbolea.
Palizi ifanyike si chini ya mara 2 –
4 kwa mwaka na miche ikifikisha miaka 3 unaweza ukasafishia miaka mitatu
unaweza ukasafishia visahani na kufyeka sehemu nyingine. Kwenye mbolea weka
samadi iliyoiva debe moja hadi mbili kwa shimo, changanya mbolea na udongo wa
kwanza kutoka shimoni, iwapo itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK
na Mijingu Phosphate changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top
soil).
Uzao.
Kuanzia miaka mitatu miche itaanza
kutoa maua na kuzaa na huchanganya kuzaa baada yamiaka mitano, miche huendelea
kuzaa hadi kufikia miaka mitano 25 – 30 tangu kupandwa.
Magonjwa na wadudu katika michungwa.
Magonjwa.
1.Vidonda katika shina.
Huletwa na aina fulani ya ukungu.
Dalili za ugonjwa huu nikutokea sehemu ya shina ambayo hubadilika rangi.
Dalili; Huongezeka ukubwa na baadae
kutoa utomvu.
Kudhibitisha; Hutokea sana sehemu
iliyo na udongo ambao huatamisha maji.
2. Ugonjwa wa kukauka miti.
Husababishwa na virusi ambavyo
husambazwa na chawa weusi.
Dalili; Sehemu ya shina hunyauka na
ndani yake hutokea mipasuko pasuko,kasha mmea hudhoofika polepole na kutoa
matunda madogo madogo, na majani hubadilika ghafla na kuwa ya njano.
3.Ugonjwa wa kutobadilika rangi kwa
machungwa yanapokomaa.
Hutokea hasa kwenye sehemu za
miinuko ya kati na kusambazwa na vidudu viitwavyo psyllids, na vile vile kwa
kuchukua vikonyo na kubebeshea kutoka kwenye miti inayoonyesha dalili za
ugonjwa.
Dalili; Hutokea mabaka ya njano
kwenye majani, pia matunda huwa ya ukali nay a njano sana.
KUZUIA:
Sehemu ambazo ugonjwa unaweza
kutokea angalia wadudu kama chawa. Hakikisha wadudu hawa hawashambulii miche
kwenye kitalu. Wakiwepo, majani huonyesha kujikunja kwa kuweka mafundo sehemu
ya juu. Vilevile epuka kuchukua vikonyo kutoka kwenye miti yenye dalili za
ugonjwa huu.
WADUDU:
1.Nzi weupe (white fly).
Hawa ni wadudu ambao hukaa kwenye
majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, na hii
husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Njia ya kiusalama zaidi ni kwa
kupandisha shambani wadudu aina ya Cales
noacki ambao huwala hawa nzi weupe na kuzuia kusambaa kwao.
2.Wadudu mafuta (aphids).
Hawa ni wadudu weusi ambao hukaa
kwenye majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, nah ii pia
husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Tumia kiuwa wadudu (insectside).
Kuvuna
Mchungwa huwa tayari kuvunwa miezi 3
– 4 baada ya kupandwa. Kuvuna ni kwa njia ya mikono au kwa kutumia kikapu cha
kuvunia.
Hifadhi
Machungwa huhifadhiwa kwenye ghala
safi lenye kuruhusu hewa. Ghala lijengwe nje ili kuruhusu hewa safi ili
yasioze.
Soko
Soko la ndani na nje ya nchi lipo.
Kiasi kikubwa cha machungwa hutumika hapa nchini, pia huuzwa nchi za jirani.
Bei ya chungwa ni shilling 200 – 300 kwa kila moja na hadi 500 hufikia
kulingana na aina ya msimu.
Hitimisho
Ili kupata mmea wa mchungwa kama
tunda ambalo linanunuliwa, huna budi kuitunza mbegu hiyo kwenye unyevunyevu
kasha tu baada yaya kuzitunza kwenye tunda na kuziotesha katikahali ya unyevu;
na pindi mmea uchipuapo hapo ukapandwe kwenye udongo kusudiwa
Comments
Post a Comment