KILIMO CHA MCHICHA:-Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili ambayo hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na madini aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya kupikwa au kutengenezwa supu.
Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili ambayo
hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na madini
aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya kupikwa au
kutengenezwa supu.
Mbegu zake zinaweza kusagwa na kupata unga
unaoweza kutumika katika mapishi mbalimbali kama vile kutengeneza ugali, uji,
chapati na maandazi. MAZINGIRA Mchicha unaweza kulimwa karibu katika aina
yeyote ya hali ya hewa na kwenye udongo wa aina yeyote ili mradi usituamishe
maji.
Udongo wenye rutuba nyingi unafaa zaidi kwa
ustawishaji wa zao hili. AINA Kuna aina nyingi za mchicha; zifuatazo ni aina
zinazostawi hapa nchini:- Mchicha Mweupe Aina hii ina majani marefu yenye rangi
ya kijani ya kupauka. Huvunwa kwa kung’oa na huuzwa sana sokoni.
Mchicha Mpana Ni ule ambao ni mnene na una
majani mapana na yenye rangi ya kijani kibichi. Huweza kuvunwa kwa
kurudiwarudiwa Mchicha Mwembamba Huu ni mdogomdogo na unaota shambani kama
gugu. Majani yake ni madogo na huchanua mapema.
Mchicha wa Unga Mchicha huu huwa mwekundu
unapokuwa mdogo na hukua haraka. Hutoa mbegu nyingi ambazo zinaweza kusagwa
unga, ambao unaweza kutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile, uji na
maandazi. Majani yake hupikwa kama mboga au hutengenezwa supu.
KUTAYARISHA SHAMBA Tayarisha shamba mwezi
mmoja kabla ya kupanda. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri ili kuongeza
rutuba ya udongo. Mbolea hizi pia hufanya udongo ushikamane vizuri na kuhifadhi
unyevu kwa muda mrefu. Weka kiasi cha ndoo moja yenye ujazo wa lita ishirini
katika eneo la mita mraba mmoja. Changanya vizuri mbolea hii na udongo.
Wiki mbili kabla ya kupanda laininsha udongo
na sawazisha udongo. KUPANDA Kuna niia kuu mbili za kuoanda mchicha, Kupanda
mchicha moja kwa moja shambani na kuotesha miche kwanza kwenye kitalu. Kupanda
Moja kwa Moja Shambani Mbegu hupandwa moja kwa moja kwenye shamba la kudumu na
baadaye mimea hupunguzwa na inayobaki huachwa katika nafasi ya sentimita 15
hadi 23. Mbegu huweza kupandwa katika sesa au matuta.
Kiasi cha kilo moja hadi mbili za mbegu
kinatosha kuotesha katika eneo la hekta moja. Ili kuepuka mlundikano wa mbegu
sehemu mmoja, changanya mbegu na mchanga kwa kiasi kinacholingana kabla ya
kumwaga shambani. Kisha mwaga na funika kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea
laini za asili. Tandaza nyasi kavu na mwagilia maji.
Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni
hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku tatu mpaka tano na baada ya
kuota ondoanyasi. Kuotesha Miche Kwenye Kitalu Kutayarisha Kitalu: Sehemu
itakayooteshwa mbegu inatakiwa iwe laini na yenye rutuba ya kutosha. Hivyo
baada ya kulima lainisha udongo kwa kupigapiga mabonge makubwa.
Kisha tengeneza tuta lenye upana wa mita moja
na urefu wowote. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha debe moja au
mbili katika kila eneo la mita mraba moja. Changanya mbolea hii na udongo
vizuri, kisha sia mbegu zilizochanganywa na mchanga kwenye mistari yenye nafasi
ya sentimita 10 hadi 15.
Baada ya kusia, funika mbegu kwa kiasi kidogo
cha udongo au mbolea laini za asili. Weka matandazo na mwagilia maji. Endelea
kumwagilia kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota. Baada ya siku 4
mpaka 6 ondoa matandazo na endelea kumwagilia maji.
Comments
Post a Comment