KUKU WA NYAMA ( BROILER)...
KUKU WA NYAMA ( BROILER)...
Kuhusiana na kuku hawa yaan broiler kwanza lazima ufahamu yafuatayo
MAANA NA SIFA ZA KUKU WA NYAMA
Kuku wa nyama huwa ni mchanganyiko wa makoo na majogoo ambao hufugwa kwa ajili ya kuuzwa kwa ajili ya nyama.
Kuku hawa hutakiwa kuwa na sifa zifuatazo.
▶ Uwezo wa kukua haraka.
Wanatakiwa waweze kufikia uzito wa kuchinjwa ndani ya kipindi cha wiki 6-8. Wakati huo wanatakiwa wawe na uzito usiopungua kilo moja na nusu.
▶ Wawe na ufanisi wa kubadili chakula kuwa nyama
Kuku wanaoweza kubadili chakula wanachokula kuwa nyama kwa ufanisi, wanasemekana kuwa na uwiano wa juu wa kubadili chakula kuwa nyama.
Uwiano huu unakokotolewa kwa kugawa uzito wa chakula kilicholiwa kwa uzito ndege mwenyewe.
Kuku mzuri wa nyama hutakiwa kuwa na uwiano wa 2.5:1
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUFANIKISHA UFUGAJI WA KUKU HAWA WA NYAMA
▶ Chagua mfumo mzuri wa kuwafuga.
Mfumo mzuri unaowafaa kuku hawa ni ule wa matandiko.
▶ Banda la kuku lijengwe mahali pazuri.
▶ Banda la kuku liwe zuri na imara.
▶ Chagua aina bora ya kuku wa nyama.
▶ Walishwe chakula bora na kiwe cha kutosha.
▶ Tunza usafi wa banda la kuku na mazingira yake.
▶ Dhibiti kuku wako dhidi ya kudonoana
▶ Weka kumbukumbu nzuri za ufugaji.
▶ Uza kuku mara wapatapo uzito unaotakiwa wa kilo moja na robo hadi moja na nusu. Uzito huu unatakiwa kufikiwa wakiwa na wiki 6-8. Wanaweza kuuzwa wakiwa hai au wakiwa nyama.

Comments
Post a Comment