Ufugaji: waliofanikiwa katika ufugaji



Image result for ufugajiKutokana na hali hiyo, madaktari wanawashauri watu kubadilisha tabia ya ulaji na kuingia katika ulaji wa nyama ya kuku wa kienyeji ili kulinda afya zao.

Joshua Buberwa na Ally Mlinga ni miongoni mwa watu walioanza kuzingatia ushauri huo, wameanza kuondokana na ulaji wa kuku wanaofugwa kwa kulishwa vyakula vilivyotengenezwa kwa mchanganyiko wa kemikali mbali mbali.

Vijana hao wanasema mbali na kutaka kuondokana na ulaji wa nyama ya kuku wanaoitwa wa kisasa, wameamua kufuga kuku wa kienyeji kwa sababu kwao mpango huo ni pia ajira.

"Mimi na rafiki yangu Ally hatuna mpango wa kutafuta ajira rasmi, ufugaji kuku wa kienyeji ndiyo kazi yetu rasmi, kwa mwezi tunapata zaidi ya Sh. milioni 2," anasema Buberwa mwenye umri wa miaka 21.

Buberwa na Mlinga ni vijana waliohitimu elimu ya Chuo Kikuu na mmoja kidato cha sita, wote kwa pamoja wameamua kuondokana na tatizo la ajira na kutumia elimu yao kwa shughuli ya ufugaji kuku wa kienyeji.

Buberwa anasema walianzisha mradi huo wakiwa na kuku 20 na sasa wanapata Sh. milioni 2.5 kwa mwezi, na baada ya kutoa matumizi ya gharama za uendeshaji wa mradi wanabaki na Sh. milioni 1.5.

Anasema mradi huo ulianza na kuku 20 mwaka 2010, lakini hadi sasa kuku hao wameongezeka na kufikia 14,000.

Aanasema uendeshaji wa mradi huo unafanyika kwa gharama nafuu kulinganisha na ufugaji wa kuku wa kisasa ambao gharama yake ni kubwa.

Anasema kupitia ufugaji wa kuku wameweza kununua magari manne,viwanja ,mashine ya kusaga na mashine ya kutotolea vifaranga vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 150.

Buberwa anasema vijana wa sasa wanatakiwa wafungue macho ili waweze kuanchana na mawazo ya kuajiriwa, badala yake wawe wabunifu kwa kufanya miradi kama ya ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Anasema kwa sasa bishara ya ufugaji huo ni kubwa kutokana na sehemu kubwa ya jamii kupendelea kula nyama ya kuku wa kienyeji.
Buberwa anasema kuku moja wa kienyeji kwa sasa anauzwa Sh. 15,000.

“Kwa kuzingatia gharama nafuu za uendeshaji, bei hiyo ina faida kubwa,” anasema.
Anasema gharama za mradi wa kufuga kuku wa kienyeji kwa maana ya muda, pia ni ndogo, kwa vile mtu anayefuga kuku wa aina hiyo hatumii muda mwingi na gharama kubwa kuwatunza.

“Mfugaji akiwa na kuku 10, baada ya miezi mitatu atakuwa nao 100 na kama watatunzwa vizuri kwa kupewa chanjo kwa wakati ndiyo idadi inaongezeka haraka,” anasema.

Anasema ukiwa na kuku 100, utakuwa na uhakika wa kupata mayai 50 kwa siku, yai moja linauzwa Sh. 300, kwa hali mfugaji wa kuku wa aina hiyo ana uhakika wakupata Sh. 15,000 kwa siku wakati gharama ya kulisha kuku hao kwa siku, haifiki kiasi hicho.

“Kipato hicho kwa siku ni sawa na Sh 450,000 kwa mwezi, hii ni sawa mshahara wa mwajiriwa serikalini mwenye elimu ya chuo kikuu” anasema Buberwa.

Anasema kuku hao wapatao 14,000 wanawafuga katika shamba lao kubwa lililoko Bagamoyo na ofisi yao iko Tegeta kibaoni, Dar es Salaam.

Anasema ufanisi wa shamba lao ni kivutio kikubwa, kwani watu mbalimbali wanatembelea siyo kununua kuku tu, bali pia wanaponunua kuku, mayai na vifaranga na wao wanaonyesha hamu ya kuiga mfano huo.

Anasema mbali na shamba la Bagamoyo lililopo kijiji cha Kimere, yeye na rafiki yake Ally pia wanakusudia kuanzisha shamba lingine la kuku wa kienyeji na mifugo mingine mkoani Morogoro.

Anasema mbali na wao wenyewe kunufaika kiuchumi, mradi wao wa ufugaji kuku umetoa elimu kwa wafugaji wadogo wapatao 200 na sasa wananunua vifaranga kwao na kuanzisha shughuli za kufuga kuku wa kienyeji. 
Watu wengi katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia wanaathirika kwa maradhi mbali mbali kwa kula vyakula vyenye sumu, kama vile baadhi ya nyama ya kuku wa kisasa.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

MAAJABU KUHUSU MAFUTA YA MAWESE

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI