UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA (6) TU!



UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA (6) TU!
(Kuku 200 x 5,000 = 1,000,000)
Unaweza ukaniona kama mimi ni kichaa na ninaye ota ndoto za mchana ambazo hazina mafanikio wala tija maana nadharia hii
inaweza isiwaingie vizuri watu vichwani mwao. Watu wengi wamekuwa wakisema na kushauri hata kushauriwa hata na wale
wasiofaa. Ninaamini wengi wetu hawapendi kuamini kile wanachoambiwa hadi pale watakapoona kwa macho yao ndipo waamini
(akina Tomaso). Sikia nikuambie! kama huamini haraka kitu chochote hebu usimkatishe tamaa yule aliyekwambia habari hizo za
kukatisha tamaa, badala yake jaribu kupeleleza na kufuatatilia hatua kwa hatua tena kwa makini maelezo uliyopewa, kisha yaweke
katika utendaji (tenda/fanya)
 kwa ufanisi kisha subiri matokeo. Baada ya kupata matokeo sasa unaweza kwenda mbele kidogo
ukauliza/kusoma/kujifunza zaidi ili kuona kama kuna mahali umekosea au hukuzingatia kanuni na maelekezo uliyopewa. Baada ya
kupata maelezo ya ziada hebu rudia kufanya tena kwa kuboresha kupitia maelekezo ya awali na hayo mapya uliyopata yote kwa
pamoja ili upime matokeo yake. Hapo sasa utakuwa upo kwenye haki ya kuamini au kutoamini kwamba jambo hilo ni kweli au siyo
kweli na siyo kutaa tu kwa ubishi usiokuwa na maana yeyote. Kwa kufanya hivi hakika utapiga hatua mbele katika kuboresha
maisha yako ya sasa na ya baadae. Ila ukifanikiwa usije ukamkufuru Mungu aliyekuwezesha.
Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana). Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula
kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani; wanga, protini, calcium, chumvichumvi,
madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/kizungu/chotara (kama nilivyoeleza
hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo).
Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda.
Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo pana usalama wa kutosha
(mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).
Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii
inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na vifaranga majogoo na mayai madogomadogo
mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike. Acha kuwawekea mayai ya mviringokama mpira!
Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/waatamie kwa pamoja.
Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako. Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila
msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku wako huku mayai mengine
yakisubiri awamu ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 = Mayai 60.
Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku
walioatamia chakula chenye viini lishe vya kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula
mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata
moja. Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende kufukuzana na panzi na vyakula
majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayaiyao.
Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga kibanda kidogo ndani ya banda kubwa ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi
kubwa na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo.
Baada ya kuku hao 5 kuangua vifaranga wako 60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea vifaranga inapoanza. Elewa kuwa ili upate
mafanikio haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea vifaranga inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza,Unatakiwa kuondoa na kuchoma
moto/kufukia mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa banda lote ili kuepusha magonjwa kama vile kuharisha, viroboto, papasi
nk. Hapo unaweza kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja kadri wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga wa mwisho,
yaani Yule wa 60 na kuwaweka katika kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na kuwawekea mayai mengine mama zao (yale 15/18
kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie tena kwa siku 21 hadi 24 zingine. Unapotoa kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia humfanya
Image result for ufugaji
kuku Yule ashindwe kutoka kwenye mayai maana hana mtoto wa kulea.
Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia maana atasubiri kupata vifaranga na
ndipo atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila wasiwasi. Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umejipatiavifaranga/kuku zaidi
ya 100 ndani ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa kuwapa chakula cha
kutosha, maji, majani ya makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate vitamini na madini mengine muhimu kwa afya zao. Fanya
hivyo hata watakapokuwa wametotoa na ukawanyang’anya vifaranga. Hii itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya maana kuku
wengi hunyonyoka manyoya wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na kisha
wataanza kutaga tena na kuatamiakama mwanzo.
Vifaranga wako hakikisha unawatengenezea chumba chao kido ndani ya banda kubwa/jikoni, kisha wawekee chanzo chochote
cha joto kama vile; taa ya chemli/jiko la mkaa/vizinga vya moto nk ili wasiathiriwe na baridi hasa wakati wa usiku. Umakini
mkubwa sana unatakiwa hapa! Hakikisha unakuwa makini wakati wa usiku ili kuongeza na kupunguza joto ndani ya kibanda cha
vifaranga maana wakati huu maranyingi joto hupungua na ubaridi huongezeka na hivyo unaweza kuua vifaranga wako.(thesolutiontz@gmail.com )

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

MAAJABU KUHUSU MAFUTA YA MAWESE

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI