UFUGAJI: njia za ufugaji wa ngombe wa kisasa na jinsi ya kupata faida yake
Tanzania
ni moja ya nchi zenye mifugo mingi Africa,
hasa ng'ombe wa kienyeji, lakini uwingi huu unaonyesha hauonekani na hauendani
sambamba na kipato cha mfugaji. Jambo hili limegubikwa na changamoto nyingi sana. Hili tutaliongelea
siku nyingine.
Leo hebu tujikite katika ufugaji wa ng'ombe wa Maziwa na
Aina zake. Tunapoongelea ng'ombe wa Maziwa tunajielekeza katika makabila ya
ng'ombe wa Maziwa wa kigeni. Makabila haya yaliingizwa na kuendelezwa hapa
nchini kitaalamu hasa miaka ya 1974 pale Mwalimu Nyerere alipoona uhitaji wake
na kwenda kuwaomba wamarekani wamsaidie, Shirika la Kimataifa la Mitamba,
HEIFER INTERNATIONAL, ndio waliopewa jukumu hilo la kusimamia mradi huo mkubwa
na ilibidi watafutiwe sehemu yenye hali ya hewa inayoendana na walikotoka.
Waliwekwa katika shamba la Kitulo na kuzalishwa na kuendelezwa pale kitaalamu.
Ng'ombe hawa hula chakula kingi na kunywa maji mengi tofauti
na wale wetu tuliowazoea wa kienyeji. Pia ng'ombe hawa si wavumilivu sana kwa magonjwa, Kwa hiyo mfugaji lazima uwe karibu sana na mfugo wako.
Katika kuhakikisha kwamba ng'ombe hawa hawapati maambukizi
ya magonjwa na wanaweza kupata chakula cha kutosha, inashauriwa wafugiwe ndani
na kuhudumiwa kila kitu ndani.
Ng'ombe hawa wakifugwa vizuri na kuhudumiwa vizuri wanaweza
wakatoa kuanzia Lita 10 hadi Lita 50 kulingana na kabila la ng'ombe. Kwa hiyo
wakulima na wafugaji wadogo wadogo wanaweza kupata maendeleo ya haraka na yenye
tija Kwa kufuga ng'ombe wa aina hii.
Katika mjadala wetu huu tutaangalia pia jinsi ya kuwaboresha
ng'ombe wa kienyeji ili kuongeza tija katika utoaji wa Maziwa.
AINA ZA NG'OMBE WA
MAZIWA.
Zipo aina tatu kuu za ng'ombe wa Maziwa ambazo ni;
i. Halisi (pure)
ii. Chotara (cross)
iii. Asilia
Ng'ombe halisi: Ng'ombe huyu ni yule asiye kuwa na
mchanganyiko wa damu ya kabila jingine.
Makabila ya Ng'ombe
Halisi.
Yapo makabila mengi ya ng'ombe wa Maziwa. Lakini kwa Afrika
mashariki yapo makabila maarufu matano;
i. Friesian
ii. Ayrshire
iii. Jersey
iv. Guernsey
v. Brown Swiss
Comments
Post a Comment