Ufugaji: Matumizi ya laki 3 300,00 kwenye mtaji

Biashara biashara, Mtaji wa kuanzia 300,000/= tu
kufuga kuku wa kienyeji;
mchanganuo:
-Tsh.60,000 kwaajili ya kujenga/kuandaa banda, chakula na virutubisho vya kuku.
-Tsh.50,000 kwaajili ya kuku wa kuanzia. Usinunue kuku wakubwa, ni ghali sana na wanakua used/wametumika sana, nunua kuku wadogowadogo waliotoka tengana na mama yao sio muda. Kwa huku (ir) bei ni tsh.5,000 so hapo utanunua kama 10 hivi. Ila make sure una mix, majogoo mawili ni tosha kabisa, vongine vijike (tetea).
-najua vitu kama maji, mtu wa kuhudumia huna haja ya kuajili mtu. Wewe mwenyewe husika maana bado ndio unaanza.
-Hadi hapo unakua umetumia Tsh.110,000 tu. Nyimgine iliobaki weka kwaajili ya backup ya madawa, chakula, pesa ya kumlipa docta (hii muhimu sana, usiwe bahili kuwalipa wale jamaa, ata kama kuku zako ziko poa kiafya, muite azicheki tu, sio gharama, akija mara moja unaweza mtoa buku 3 hivi fresh)
-Kuku (hao madogo ulionunua ambao umri wao ni kama miezi 4 hivi) watachukua tena kama miezi 2 ili waanze kutaga au ata kuuza. Hapo pesa itaanza kuzunguka.
Baada ya hii stage, hujamaiza:
-unaweza anza na kufuga kuku wa mayai, wale ambao hawaatamii mayai. Hapa utaanza pata mayai na kuyauza. Hivyo utakua unapiga pesa kwenye mayai na kuku.
-Unaweza pia ukanunua na zile mashine za kutotoleshea vifaranga(bei zake ni kama 80k hivi, ila lazima kuwe na umeme unapokaa).
Hitimisho;
-ukianza leo najua baada ya muda kama wa miezi 8 unaanza kupiga hela ya mayai na nyama.
Pesa ulionayo sasa (laki 3) usijidanganye ukaanzisha duka, genge, au biashara za uchuuzi wa mazao au vitu toka mjini upeleke kijijini. Hizo waachie wenye pesa ndefu, ambao ata shoti (hasara) ya laki 5 ikitokea hawayumbi. Wewe hapo ukipoteza/ukipata hasara ya laki 1 tu, kuirudisha daah itachukua muda.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze kuhusu mbilimbili na matumizi yake yote

MAAJABU KUHUSU MAFUTA YA MAWESE

JUA KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI