Je unajua ni vitu gani muhimu katika ujenzi wa banda bora tupe maoni yako nasi tukufungue sasa
UJENZI WA MABANDA BORA YA KUKU : Banda lifaalo lazima liwape kuku mazingira mazuri na kuwalinda dhidi ya hali mbaya ya hewa (mvua, upepo na jua). Hakikisha banda lina nafasi ya kutosha kwa kuku wanaofugiwa humo. – Uwiano mzuri wa kuku kwa eneo ni futi mraba moja kwa kuku wa mayai, na futi moja ya mraba kwa kuku wa nyama. Kwa sehemu za tropiki mabanda yawe wazi sehemu za juu ili kuruhusu mzunguko wa hewa, Pia liwe na mwelekeo wa mashariki-magharibi ili kupunguza kiasi cha mwanga wa jua kuingia moja kwa moja katika banda. – Ni muhimu banda iwe muonekano wa mstatiri na ukuta wenye kimo kisichozidi futi tatu kwa upande mrefu. Ukuta huu unaweza kutengenezwa kwa mabati yaliyokatwa au mbao za rangi ya fedha au matofali. Pande zilizobaki za kuta ziwekwe wavu wa waya. Paa la banda lazima liweze kuakisi mwanga na joto. Haya yote yatasaidia katika kuhakikisha kwamba banda liko katika hali nzuri linastahili kufugia. – Sakafu imara ya sementi ni bora kwa sababu ni rahisi kusafishwa. Laz...