Posts
Showing posts from January, 2018
MAGONJWA YA KWALE NA JINSI YA KUPAMBANA NAYO
- Get link
- X
- Other Apps
Magonjwa KWALE ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata KWALE ni typhoid, mafua na kuharisha . Tiba za asili Waweza kuwatibu vifaranga au KWALE wako kwa kutumia njia ya asili ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama. Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa KWALE na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara. Mwarobaini na Aloe Vera: Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya KWALE. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika ma...