JUA JINSI YA KUANDAA MICHE YA MIPAPAI
Uandaaji wa mbegu za mipapai imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watu, leo nitaongelea uaandaaji wake mpaka kupanda na kupata miche yako Mbegu tulizotumia leo ni LADY RED ambazo hufaahamika zaidi kama Malkia FI toka nchini Taiwan na huzalishwa na kampuni inayojulikana kama KNOWN-YOU kama zinavyoonekana hapo pichani Fungua mbegu zako na uziweke kwenye chombo kisafi kisha jaza maji kiasi, ziloweke humo kwa siku 5 na kila siku badilisha maji Siku ya 6 zitoe na uziweke kwenye kitambaa kisafi kukwepa mashambulizi ya fangas, Funga vizuri na lowesha maji kitambaa chako na ukihifadhi sehemu salama Zoezi hili linatakiwa kufanyika ndani ya nyumba au banda ambalo litazikinga mbegu dhidi ya jua la moja kwa moja Siku ya 7 ukifungua utaona baadhi ya mbegu zimeanza kupasuka na tayari kwa kuanza kuota, panda mbegu zako moja moja kwenye viriba ambavyo ulishaviaandaa kabla kwa kuvijaza udongo wenye rutuba, kama utaweka mbolea hakikisha ...