KILIMO. kilimo bora cha korosho
UTANGULIZI koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16 century ndipo lilipo fika africa katika nchi ya mozamboque na baadae likafika Kenya na Tanzania. kwa hapa Tanzania korosho ulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji. mvua; korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka, napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari. udongo; korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga. KUANDAA SHAMBA kama mazao mengine shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho. nakatika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba. KUPANDA Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu utakayo panda ndo itakuonesha kiasi gani utavuna, baada ya kununua mbegu...